Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Muda ni sehemu ya ulimwengu. Hakuna wakati ulimwengu haukuwepo kwa sababu muda ulianza pale ulimwengu ulipoanza.
Ulimwengu haukuanza.

Muda upo ndani ya ulimwengu.

Muda unapita ndani ya ulimwengu, Lakini Ulimwengu unaendelea kuwepo tu.

Ulimwengu umekuwepo milele. Haukuanza.

Ulimwengu umekuwepo, upo na utaendelea kuwepo milele.
Kabla ya hapo kulikuwa na timelessness hali isiyo na muda.
Hiyo hali isiyo na muda ilikuwa kwenye nini?
Na kilichosababisha muda uanze lazima kiwe kiko nje ya muda. Huyo ndio Mungu.
Muda upo ndani ya ulimwengu ambao haukuanza.

Huyo Mungu hayupo na hajawahi kuwepo.
Soma fizikia uache kukariri maneno ya vijiweni.
Usifosi imani zako uchwara ulizopumbazwa.
 
huenda upo sahih kila kitu kinapotokea kimesababishwa asili ya mwanadamu ni ipi kama hajaubwa?
Asili ya mwanadamu ni wazazi wake.

Kila binadamu kazaliwa na wazazi wake.

Na wazazi ndio asili.

Sasa sijui nyie mnataka asili gani nyingine?
 
Unajisifu wakati huna hoja
Kama upo makini kichwani
Subiri watu wakusifie

Nionyeshe hilo jibu
Nalisubiria
Mr Misifa.
 
Rudia kusoma halafu ujibu tena, maana ni wazi haujaelewa nilicho kiandika.
 
Ni kweli sawa na wale wanaoamini Mungu.
 
Unajisifu wakati huna hoja
Kama upo makini kichwani
Subiri watu wakusifie

Nionyeshe hilo jibu
Nalisubiria
Mr Misifa.
Hahaha hauna hoja bhana, hakuna sehemu umejibu hoja zangu za nyuma hizo.

Unataka upewe hoja ili hali wewe unaandika madudu binti? Unapenda kutongozwa eh?
 
Sayansi inafundisha kukubali jibu lililopitia uchunguzi unao pimika.

Ndio maana tuna wana sayansi wanaoamini Mungu lakini hatuna Sayansi inayokubali dhana ya Mungu.

Wewe kumuweka Mungu kama chanzo cha kwanza si uthibitisho wa kumfanya awepo, hiyo ni personal choice ambayo haikufanyi uwe tofauti na mwingine anayesema Unicorn wapo.

Kitachoweza kukutenganisha wewe na huyo mwingine, sio mkusanyiko wa makaratasi yaliyopewa jina Biblia.

Ni uthibitisho usioacha shaka unaoonesha huyo uliyemuweka kama chanzo cha kwanzo ni kweli yupo.
 
tunataka kujua wale wazazi wa kwanza walitokea tu? Wakawa wazazi au walitoka wap?
Wazazi wa kwanza kina nani?

Kama origin ya binadamu wote ulimwenguni ni wazazi wawili tu wa kwanza, Iweje sasa binadamu tuna tofautiana rangi na vinasaba?

Ikiwa origin yetu ni mtu mmoja wa mwanzo, Kwa nini kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea, wahindi?

Je hao wazazi wa mwanzo walikuwa weupe au weusi?

Huoni kwamba hakuna Wazazi wa mwanzo wa binadamu wote ulimwenguni?

Kama ingelikuwa tumetokana na Wazazi wawili tu wa mwanzo, Basi binadamu wote ulimwenguni tungefanana kwenye rangi.

Lakini tuna tofautiana. Kwa hivyo hatuja tokana na wazazi wa mwanzo.
 
Sheria ya mantiki inasema everything that begins to exist has a cause, ulimwengu una mwanzo hivyo unahitaji chanzo. Mungu hana mwanzo, Yeye ni eternal, hivyo hahitaji chanzo.
Kwanza hakuna sheria ya mantiki ya kisayansi inayosema hivyo, hiyo ni theological argument tu.

Hakuna uthibitisho ulimwengu kuwa na mwanzo au chanzo.

Hata kama ulimwengu ungekuwa na mwanzo hakuna uthibitisho ungehitaji chanzo.

Hata kama kuna chanzo hakuna uthibitisho hicho chanzo ni mungu.

Pia cause sio sawa na creator
 
Huyu ndio masikini wa kutupwa kabisa hivi wewe ulishawi kufuga hata kuku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…