Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Mateso tunayoyapata duniani kuanzia vita, magonjwa ni zaidi ya huo moto.


Hivi unadhani pale Congo Kuna mtu kuanzia kazaliwa Hadi anakufa ni vita Kila siku utamtisha kuhusu moto.
 
Hata bila vipimo uwepo wa mungu (Abrahamic God) unaonekena hauwezekani kwa sababu ya "contradictions". Mfano anasemwa ni mwema na mwenye nguvu zote lakini ameumba au ameruhusu ulimwengu wenye mateso, magonjwa, vifo, ajali na majanga.
 
Alie muumba anamuhusu yeye. Mimi anae ni husu ni huyu alieniumba
Hakuna binadamu alieumbwa


Wewe ulizaliwa baada ya baba yako kummwagia shahawa mama yako ndio wewe ukatungwa. Hakuna sehemu Dunia hii binadamu anaumbwa.
 
Ila wewe Mungu wako si amekupa amri kuwa usiibe, unapata nguvu ipi kuhalalisha kuwa kudhulumiwa sio kosa
 
Kwamba wale watu wanaoenda Kwa MWAMPOSA Kununua udongo Ili wapate Fedha na kupona magonjwa ni watimilifu wa akili kuliko atheist anaehoji uwepo wa Mungu.
 
Wanasayansi wanamtambua mungu yupi? Jehovah, Allah, Brahma au Pangu ?
 
Soma kitabu kinaitwa God is not great by Christopher Hitchens, utapata akili kidogo
 
Unamuita mtu alieumbwa Kwa mfano wa huyo Mungu wako muweza wa yote kichwa ngumu. Mtu alieumbwa Kwa mfano wa Mungu kichwa ngumu.

Kama Mungu anashindwa kutengeneza binadamu asiekuwa na kichwa ngumu ataweza wapi kutengeneza mifumo complex ya kidunia.
 
Mwanasayansi kusema Mungu yupo haimaanishi Mungu yupo bila evidence.
Pia mungu hawi hayupo kwa sababu hakuna evidence....kuna vitu vingi vimegundulika kisayansi ila siyo kwamba vimeanza kuwepo baada ya kugundulika la ..niliwaambia kina kiranga hapa jf kuwa sayandi is reverse engeenier or reverse knowledge of God creation..vitu vyote vilivyo gunduliwa kisayansi vilikuwepo kabla hata ya wanasayansi kuvigundua ...NA MUNGU NI HIVYO HIVYO.
 
Wanasayansi wanamtambua mungu yupi? Jehovah, Allah, Brahma au Pangu ?
Hilo swali linatokana na wewe kushindwa kujua mungu ni nini ? Mungu ni nguvu za asili zenye akili na ufahamu zilixo umba vitu vyote ....na wanasayansi wanakubali kuwa nguvu za asili ndiyo chanzo cha vitu vyote ..ila wanacho jaribu kukanusha au kuficha ni kuhusu kuwa nguvu hizo za asili zina akili na ufahamu wao wanadai kuwa nguvu za asili ziliumba vitu kwa bahati tu ..jambo ambalo kamwe aliwezi kuwa sahihi kisayansi kwa sababu ukitazama hata kiumbe kama binadamu kimeumbwa kwa akili na ufahamu wa hali ya juu kabisa siyo kibahati ....
 
Kuna Miungu zaidi ya 10,000 duniani , Je ni Mungu yupi anaeelezeka kisayansi?

Kwa mfano Mungu wa Islam na Mungu wa ukristo !
 
Chanzo cha huyo mungu ni nini/kipi ?
 
Kuna Miungu zaidi ya 10,000 duniani , Je ni Mungu yupi anaeelezeka kisayansi?

Kwa mfano Mungu wa Islam na Mungu wa ukristo !
Hapa tunazungumzia mungu yupo au la ! Mfano kuna swali na watu wakaja na majibu mengi kwenye swali moja ..hii aina maana kuwa hilo swali halina jibu la...bali ni watu waliokuja na majibu mengi ila jibu lipo ...hivyo Mungu muumba wa yote yupo ila ni Mungu yupi,? hapo ndiyo kunakuja itikadi za dini.
 
Usichanganye mystery na evidence. Kitu kuwa hakijaelezeka hakumfanyi Mungu kuwa explanation. Kama hatujui kwa nini kitu fulani kipo, jibu la kwanza la kimantiki ni “hatujui bado,” si “kwa hiyo Mungu ndiye aliyekifanya.” Vinginevyo kila pengo katika knowledge yetu lingekuwa ushahidi wa Mungu, na kila tunapogundua explanation mpya Mungu angekuwa anasukumwa hatua moja nyuma. Hii ndiyo tatizo la God of the gaps: unatumia kile ambacho bado hatujui kama ushahidi wa kile unachokiamini. Lakini unknown ni unknown. Hauwezi kuipa jina la Mungu halafu ukadai umeupata ukweli.

Na zaidi, kusema “kuna swali ambalo halijajibiwa” hakuthibitishi kwamba jibu lake ni Mungu. Kutokujua jibu ni nafasi ya maarifa, wakati kusema “Mungu ndiye jibu” ni claim mpya inayohitaji justification yake yenyewe. Huwezi kutumia mystery kama evidence ya conclusion unayotaka kufikia.

Kwa kifupi, kutokujua si ushahidi wa Mungu; ni ushahidi kwamba bado hatujui. Na kama unataka kutoka kwenye “hatujui” kwenda kwenye “Mungu ndiye,” unatakiwa kuonyesha hatua ya kimantiki na evidence inayokupeleka huko. Bila hiyo, umebadilisha tu “sijui” kuwa “Mungu,” si kwamba umeeleza mystery.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…