Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 12,096
- 22,468
Nilimisquote na huo ni ushahidi Mungu wenu anaejua ya mbele yangu hayupo.View attachment 3651319Angalia unavyo jichanganya mdogo wangu ππ, uko frustrated.
Unatakiwa uelewe uovu kwenye jamii unatokana na watu. Ili Mungu afute uovu kwenye jamii hii ya sasa, inabidi awafute watu wote wenye mawazo mabaya, waongo, wambea, wezi, na wenye chuki.Sina uhakika kama Wakristo wote wanaamini peponi/ mbinguni ni ulimwengu au nje ya ulimwengu. Nafahamu mashahidi wa Yehova ndio wanaamini hivi.
Tuachane na huo ulimwengu wa kufikirika tuongolee huu wa sasa ulio halisi, mungu anaweza kuondoa uovu katika jamii ulimwengu huu wa sasa ulio halisi?
chimbuko la binadamu ni lipi ilikuweje mpaka kikapatikana kiumbe ambacho ni binadamu maana tunajua ukichaganya siment, mchanga, na kokoto unapata zenge je binadamu alitokea tu? Na mawe miti n.k vililetwa na nan dunian?Nimeshakwambia asili ya Binadamu ni Binadamu.
Asili ya sokwe ni sokwe.
Asili ya mnyoo ni mnyoo.
Unataka asili gani nyingine?
Sio kwamba uovu unatokana na Shetani ?Unatakiwa uelewe uovu kwenye jamii unatokana na watu. Ili Mungu afute uovu kwenye jamii hii ya sasa, inabidi awafute watu wote wenye mawazo mabaya, waongo, wambea, wezi, na wenye chuki.
Ndiyo maana nikatoa ile hoja kwamba, kuuondoa uovu ni pamoja na kukuondoa na wewe binadamu pia.
Shetani anashawishi tu, lakini maamuzi ya mwisho ni yako. Acha kumsingizia shetani udhaifu wako!Sio kwamba uovu unatokana na Shetani ?
Vipi kuhusu matetemeko ya ardhi yanayoua watu ?
Kwa hiyo hata shetani akiondolewa au asingekuwepo uovu bado utakuwepo tu ?Shetani anashawishi tu, lakini maamuzi ya mwisho ni yako. Acha kumsingizia shetani udhaifu wako!
πBasi sawa huyo kakuumba wewe peke yako. Mimi hajaniumba.
Kwa nini mungu anaruhusu yaue watu kwa maelfu ?Hayo matetemeko ya ardhi sio uovu, ni jiografia ya kawaida ya sayari yetu kuwa hai.
Ndio uovu bado ungejaa tele kwa sababu ya watu kama wewe.Kwa hiyo hata shetani akiondolewa au asingekuwepo uovu bado utakuwepo tu ?
Mbona hulaumu Mungu kuleta mvua inayozalisha chakula cha kulisha mamilioni ya watu?Kwa nini mungu anaruhusu yaue watu kwa maelfu ?
Sawa, tukubali kwamba tetemeko lenyewe si UOVU kwa sababu ni natural event. Lakini tatizo si kuLitaja tetemeko kuwa mwovu. Tatizo ni matokeo yake kwa viumbe wenye uwezo wa kuhisi maumivu na mateso.Shetani anashawishi tu, lakini maamuzi ya mwisho ni yako. Acha kumsingizia shetani udhaifu wako!
Hayo matetemeko ya ardhi sio uovu, ni jiografia ya kawaida ya sayari yetu kuwa hai.
Kwa sababu Mbeya ni jambo zuriMbona hulaumu Mungu kuleta mvua inayozalisha chakula cha kulisha mamilioni ya watu?
Huwezi kuwa na sheria za asili zinazochagua nani wa kumdhuru.Sawa, tukubali kwamba tetemeko lenyewe si UOVU kwa sababu ni natural event. Lakini tatizo si kuLitaja tetemeko kuwa mwovu. Tatizo ni matokeo yake kwa viumbe wenye uwezo wa kuhisi maumivu na mateso.
Mtoto anayekufa kwenye tetemeko hajafanya uamuzi wowote, hajachagua dhambi, wala hajamsingizia Shetani. Ameangukiwa na jengo na kufa. Sasa kama Mungu aliumba hiyo nature, anaijua kila itakachotokea, na ana uwezo wa yote, kwa nini ameruhusu mfumo wa asili ambao unazalisha mateso kama hayo?
Huko mwingine ngoja aje kukujibu mwenyewe.
Kama Mungu anaweza kutoa mvua na jua, kwa nini hawezi kuhakikisha mtoto anakula kabla hajafa kwa njaa?Mbona hulaumu Mungu kuleta mvua inayozalisha chakula cha kulisha mamilioni ya watu?
Mvua ni nzuri? nenda kawaulize watu waliokumbwa na El Nino kama wanakubaliana na wewe.Kwa sababu Mbeya ni jambo zuri
Dini gani hiyo inayoamini shetani sio chanzo cha maovu na mateso ?Ndio uovu bado ungejaa tele kwa sababu ya watu kama wewe.
Kama hakuna Mungu, Michael Jackson alikuwa anafanya jambo jema kwa nani?Kama Mungu anaweza kutoa mvua na jua, kwa nini hawezi kuhakikisha mtoto anakula kabla hajafa kwa njaa?
Kuna watoto Hadi Leo wanakufa Kwa kukosa chakula. Mungu alikuwa wapi Hadi Michael Jackson anachangisha pesa za baa la njaa Ethiopia.
Mungu mwenye uwezo wote, anayejua yote na anayewapenda wote, kwa nini anaweka mfumo ambao mtoto asiye na hatia anaweza kufa kwa njaa wakati ana uwezo wa kuzuia hilo?
Kwahiyo Mungu mwenye upendo kaweka sheria za asili za kudhuru mtu yoyote Hadi watoto wachanga wasio na hatia wauawe na Matetemeko ya ardhi.Huwezi kuwa na sheria za asili zinazochagua nani wa kumdhuru.
Nashangaa sana wanaoamini huu upuuzi πZaidi ya hayo kichekesho ni ,
kama Mungu anajua kabla mtu hajazaliwa kwamba mtu huyo atamkataa, ataishi dhambini na ataishia motoni, lakini bado Mungu anamleta duniani huku akiwa na uwezo wa kuzuia hiyo outcome. kwa nini amuumbe mtu ambaye tayari anajua ataishia kwenye eternal punishment?
Yani unamuumba binadamu unajua atakuja kuua watu, halafu huyo mtu akiua unasema utamchoma moto.
Hizi akili waumini wa MWAMPOSA ndio wanaweza kuelewa.Ll