Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Unatumia maneno aliandika Isaya au Yohana miaka 2000 iliyopita kana kwamba huwezi kutumia kichwa chako kufikiri.

Mtumwa wewe!
 



Indeed, umejilenga

Mtandaoni Darwinism ipo na wala si memes... study more or peruse internet manake wabatwuka mno na kejeli zisizo na msingi wala wa kielimu
Darwinism theory inajenga Kwa evidence za common ancestry, natural selection, genetic mutations, au ushahidi wa fossils na genetics.


Umeombwa uchague dimension ipi kati ya hizo uanze kuichallenge unaleta story.


Lete evidence kuwa binadamu alitokana na nyani based on darwinism theory na sio janja janja!
 
Unatumia maneno aliandika Isaya au Yohana miaka 2000 iliyopita kana kwamba huwezi kutumia kichwa chako kufikiri.

Mtumwa we
Unapoyaondoa maandiko ukategemea mawazo yako kwenye kufasiri Ahadi ya Mungu lazima utapishana na gari la mshahara kama walivyokuwa wayahudi apo mwanzo. note it takes a golddiger to recognize a true Gold. kama wew unatafuta kumjua Mungu kupitia maandiko utampata (math 5:6). na kama umeridhika na hicho unachokijua then uwezi pata zaidi.
 
Kama Mungu ametupa akili ya kutafuta ukweli, kwa nini Mimi nikitumia hiyo akili kuhoji maandiko iwe tatizo? Kama maandiko ni kweli, basi yanapaswa kustahimili uchunguzi wa akili si kutaka nikubali kwanza ndipo niruhusiwe.


Usitumie biblia kuthibitisha mamlaka ya biblia. Kwanza thibitisha kwa nini kitabu hicho kinapaswa kupewa mamlaka; baada ya hapo ndipo tafsiri zake ziwe na uzito.
 
Nieleweshe Kwa kunipa evidence alipo mjenzi wa Dunia kama sisi tunavyoweza kukupa evidence za mjenzi wa nyumba.
Katika hayo ulioandika unahitaji nini? Ushahidi upate kujua? Au unahitaji kujua upate ushahidi?
 
Kazi ya kuthibitisha ni yakwako na wala si mtu mwingine, lakini kumbuka maandiko ni sheria ya Mungu na sheria siku zote hufasiriwa na sheria na wala si mawazo ya watu. Maana kama ingekuwa rahisi hivyo basi leo wakristo wote ulimwenguni wangekuwa na kauli moja. strange
 
Wewe ndiye unayedai kwamba maandiko ni sheria ya Mungu, kwa hiyo ni jukumu lako kuonyesha kwa nini ni sheria ya Mungu; si jukumu langu kuthibitisha kwamba si sheria ya Mungu.


Sawa maandiko ni Sheria za Mungu, Je ni Mungu yupi ? Maana duniani Kuna Dini zaidi ya 10,000 na Kila dini Ina Mungu wake ?
 
Katika hayo ulioandika unahitaji nini? Ushahidi upate kujua? Au unahitaji kujua upate ushahidi?
Nahitaji ushahidi ili nifikie kwenye conclusion ya kwamba Mungu ndio aliumbw Dunia kama ulivyosema.

Nkiona nyumba, najua imejengwa na fundi kwa sababu nina evidence independent. Ninajua nyumba hutejengwa na watu, na ninaweza kumwona au kumfuatilia aliyeijenga.

Sasa kwenye dunia, wewe unadai kuna Muumba nyuma yake. ni evidence gani ilikupeleka kwenye conclusion kwamba Mungu ndio mjenzi wa Dunia.

Wewe ndio mwenye claim hivyo basi burden of proof Iko upande wako sio Mimi.

Unasema Tundu lisu ni Gaid wewe ndio inabidi utoe evidence.
 
Nichukuwe huu mfano wako na hapa nanukuu" Unasema Tundu lisu ni Gaidi wewe ndio inabidi utoe evidence."

Kwenye maelezo yangu nimesema nyuma ya ulimwengu angalau vitu vya asili vinavyoooneka kuna "Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili" tunaouita Mungu.

Sababu za kufikia hitimisho hilo ni jinsi gani ulimwengu ulivyotokea; ulivyo na mpangilio na muundo, unavyofanya kazi na unavyoendelea.

Aidha, (sababu nyingine) ni maarifa ya binadamu. Maafia ya binadamu yana asili ya huo Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili (Mungu).

Binadamu ameweza kuunda mitambo baada ya kuangalia vitu vya asili jinsi vinavyofanya kazi. Amejifunza sheria za fizikia; akajifunza viumbe hai jinsi vinafanya kazi akaunda mitambo mbalimbali.

Kwa lugha rahisi ameiga vitu vya asili kuunda vifaa mbalimbali.
 
Nyuma ya huo uwepo wa hali ya juu wenye akili mnaouita mungu kuna nini?
Chanzo cha huo uwepo wenye akili ni nini au kipi ?
 
Na kama tulikuwepo milele kabla ya kuwa binadamu, Mungu alituumba kweli au alibadilisha tu kitu ambacho tayari kilikuwepo milele kuwa form nyingine? Hapo ndipo nataka unieleze vizuri.
Ndiyo alituumba kutokana na nguvu(energy) za mungu zilizopo ...yaani uumbaji wa Mungu maana yake ni art of energy" katika kanuni ile ile ya energy can change from one for to another.
 
Nahitaji ushahidi ili nifikie kwenye conclusion ya kwamba Mungu ndio aliumbw Dunia kama ulivyosema.
Kuna tatizo kwenye hili.
Tatizo la 1. Ushahidi kwa wenyewe sio ukweli. Ushahidi unaweza kuwa wa uongo au ukweli.
Tatizo la 2. Ushahidi unategemea "Kujua". Kujua kunatangulia ushahidi.

Ubongo anaanza kujua unafuatia ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…