Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Msela... soma biblia uielewe, usikumbatie wasemayo wachungaji - ni binadamu hao na huwa wanakosea...

Shetani kazi yake kuu ni kushindana na Mungu kwamba aeza kuwageuza watu wake wote wamfuate yeye...
Anafanikiwa na baadhi, ila anashindwa kwa waliokomaa kiimani. Mungu katupa kipaji cha kuchagua, na anataka wafuasi waliochagua kumuumini na kufuata matakwa yake. HUU UWEZO WA KUCHAGUA NDO SABABU KUU ANARUHUSU MAJARIBIO... kama mateso ni sehemu ya majaribio kama ilivokuwa kwa Ayubu, basi anaacha na iwe, ila mwishowe anakuponya na kukubariki maradufu kama huu mfano wa Ayubu.

Therefore, kukujibu directly... umeandika Mungu alimpa amri shetani kumtesa Ayubu????? Hapana, aliruhusu majaribio na wala hakutoa amri hiyo.

Pia Kama shetani alikuwepo bustani ya Eden, we umeanzia wapi kuwazia hakuwepo duniani wakati anamjaribu Ayubu ????
 
Watu wagumu sana kuelewa kiongozi. Katika mambo ya maana kutokea ni ku barinwash watu wengi sana kuhusu haya mambo
Sana mkuu... cha kuchekesha mambo ya darwinism na big bang theory hayana ushahidi ivo ni ya imani ya msomi kwamba elimu ni foolproof... kumbe elimu mara nyingine nia yake kukufool
 
Nani aliandika Biblia?
Utakuta biblia inasema ... maandishi according to fulani , Eliya, Danieli, Yohana ama wengineo
Swali lako ni kama kuuliza nani kaandika historia ya Kinjeketile na vita vya majimaji, ama historia ya vita vya Chifu Mkwawa na wajerumani. Waliandika wao?

watu weusi, hata bibliani tulikuwa na mila ya watu spesheli ambao kazi yao maishani ni kupokea elimu flani, kukariri, na kuisimulia kwa vizazi vijavyo... ORATORS IN ORAL TRADITION. Baadae sana maandishi yanapoweza kuchapishwa ndo mwingine anaandika...

Pia Biblia ya kale ipo Ethiopia ... uwezekano wa kwenda na kutafsiri na kuandika upo vizuri tu.
 
Unaniambia nisome biblia nielewe wakati biblia yenyewe haieleweki na imekaa contradictions kuliko vitabu vya Nyambali Nyangwine.
 
Piga longo longo


Maneno meeeeeengi

Unamaliza miti tu


Lete ushahidi wa Mungu aliumba binadamu
 
Watu mnaopinga mada ni kwamba hamkubali uwepo wa huyu Abrahamic God au mnapinga idea ya kwamba kuna Mungu yeyote ambaye ana nguvu na akili kuliko chochote kwenye huu ulimwengu!
 
Watu mnaopinga mada ni kwamba hamkubali uwepo wa huyu Abrahamic God au mnapinga idea ya kwamba kuna Mungu yeyote ambaye ana nguvu na akili kuliko chochote kwenye huu ulimwengu!
We taja sifa za mungu unayemwamini,tukupe hoja kwanini huyo mungu hawezi kuwepo
 
Your browser is not able to play this audio.


Nimetembea na hata kubishana na wachungaji... ila nilipojifundisha nje ya wachungaji na kutafakari... SIONI MWINGINE WA KUABUDIWA... PRAISES BE UNTO YAH (JAH)
 
Kim Jong Jr

Sikutaka kuingiza hii ndani ya mada ila ulivoshikilia 'genetic ancestry' zetu kwa masokwe kama Darwinism inavotuambia... ntaliingiza

Kama Darwin aliongelea wao wazungu basi kwa kiasi flani yuko sahihi... DNA za wazungu wengi ka si wote zina DNA ya Neanderthals (wale masokwe mtu waloishi mapangoni ulaya). ILA SISI WEUSI TUSIO MCHANGANYIKENI HATUNA. Kwa hiyo sisi tuliumbwa na Mola Mungu.

Pamoja na sayansi kuthibitisha hizi tofauti za DNA, pia kimantiki angalia nani ana vinyweleo kibao asiponyoa hugubikwa navo ka masokwe
 
Swali ulilouliza lilikuwa rahisi sana sema kwakuwa umejijibu mwenyew umejipendelea TUNAONA vitanda vinatengenezwa na mafundi Yani ipo hivyo je wew ulishawahi kuona Allah amemtengeneza mtu?
 
Mafundi vitanda wanajulikana hata ukihitaji walipo unapelekwa na unaonyeshwa..!!

Kama mimi wangu yupo Keko

Wewe tuonyeshe mungu sasa yuko wapi niende akaniongezee hips..!!
 
Nilikuwa sijaona hii comment yako,

Tukumbushane tu wewe ulisema tumeumbwa na Mungu, lakini unatumia Neanderthal DNA kupinga wazo la Darwinism kuhusu common ancestry Ambayo sisi tunaisapot kama Moja ya vyanzo vya binadamu.

Sasa tukubaliane kwenye jambo moja......Neanderthal DNA si ushahidi kwamba Wazungu walitoka kwa masokwe.
Neanderthals hawakuwa sokwe wa leo..... walikuwa population ya kale iliyohusiana na Homo sapiens, na kulikuwa na gene flow kati yao na baadhi ya Homo sapiens.

kwa nini Neanderthal DNA iwe challenged kwa evolution? Kwa mtazamo wa evolution, hiyo DNA ndiyo moja ya evidence ya historia ya mchanganyiko kati ya populations za kale.

Kama unakataa evolution, sawa. Lakini onyesha ni wapi evidence hiyo inapingana na evolution. Kusema Wazungu wana Neanderthal DNA, kwa hiyo wametoka kwa masokwe ni tafsiri ambayo evolution yenyewe haisemi. Unaleta mameko yako.

Usipinge Darwinism kwa version ya sokwe, Pinga common ancestry yenyewe, na uonyeshe kwa nini evidence yake haikubaliki.
 
ila hauko sahihi ...mbegu shahawani si kiumbe hadi zikutane na yai ndo zitengeneze mtu / kiumbe
Sasa hapo ndipo unajijibu mwenyewe. Umesema sperm peke yake si kiumbe, na yai peke yake si kiumbe kipya; zinapokutana ndipo zinaunda zygote, ambayo huendelea kuwa human organism.

Je binadamu wa kwanza huyo Mungu wenu alizaa Kwa kufuata huo mchakato ?
 





Na muda wa kuwa hawamuabudu Muumba wao, nyoyo zao hazitapata utulivu mpaka wamuabudu Muumba wao bila ya kumshirikisha na chochote kile.


Allah Akulipe Kheri Sheikh wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…