Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumapili imemteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi makamu wa rais wa shirikisho hilo.
Nyamlani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Wambura kufungiwa maisha kujihusisha na soka.
Wambura amefungiwa na kamati ya maadili ambayo imeeleza kumtia hatiani na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi.
Hata hivyo, tayari Wambura amekata rufaa kupinga hukumu hiyo akisisitiza hakubaliani nayo.
View attachment 724736