Athumani Salum Matenga Mwana TANU Wa Tawi La Ali Masham

Athumani Salum Matenga Mwana TANU Wa Tawi La Ali Masham

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ATHMANI SALUM MATENGA MWANA TANU WA TAWU LA ALI MSHAM

Mzee Athumani Salum Matenga hivi sasa umri wake unakisiwa kufikia miaka 90.

Anasema alikuwa mwanakamati wa tawi la TANU lililoanzishwa na Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa.

Nyumba ya Mzee Athumani Matenga Mtaa wa Mwinyimkuu haipo mbali na nyumba ya Ali Msham.

Leo nilifika nyumbani kwake baada ya kufahamishwa kuwa inawezekana yeye kuwa mmoja wa wanachama wachache wa TANU walio hai si tu wa tawi la Ali Msham bali TANU yenyewe.

Mzee Salum Matenga anasema Ali Msham na Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika walikuwa kama mtu na rafiki yake na Nyerere akifika kwenye tawi lile mara kwa mara.

Mzee Athumani Salum Matenga anakumbuka kwenda uwanja wa ndege kumpokea Nyerere akiwa kwenye msafara mkubwa wa watu wengi sana akiendesha pikipiki yake siku aliporudi UNO safari ya kwanza mwaka wa 1955.

.
20201120_154034.jpg
 
ATHUMANI SALUM MATENGA MWANA TANU WA TAWI LA ALI MSHAM MAGOMENI MAPIPA

Mzee Athumani Salum Matenga hivi sasa umri wake unakisiwa kufikia miaka 90.

Anasema alikuwa mwanakamati wa tawi la TANU lililoanzishwa na Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa.

Nyumba ya Mzee Athumani Matenga Mtaa wa Mwinyimkuu haipo mbali na nyumba ya Ali Msham.

Mzee Athumani Salum Matenga na yeye kama alivyokuwa Ali Msham alikuwa seremala.

Leo nilifika nyumbani kwake baada ya kufahamishwa kuwa inawezekana yeye kuwa mmoja wa wanachama wachache wa TANU walio hai si tu wa tawi la Ali Msham bali TANU yenyewe.

Mzee Salum Matenga anasema Ali Msham na Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika walikuwa kama mtu na rafiki yake na Nyerere akifika kwenye tawi lile mara kwa mara.View attachment 1630769
Mzee MS hii inaendelea au ndio mwisho?
 
Back
Top Bottom