Ati nini? Tume huru; asubuhi na mapema!

Ati nini? Tume huru; asubuhi na mapema!

NGUCHILO

New Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
3
Reaction score
0
Skia!
Enyi mlio jirani nae, mwambieni asiogope, mstueni janja yao wanajua hawana chao. Mwambieni ukweli kwamba the so calledTume Huru (TH)” hiyo kwake ni mbachao, amkumbatie aende nae awaachie msala wao.

Wanatambua hawawezi na hawajui walitakalo, wameishiwa hadi nauli na chomboni wameshaingia. Wamepata kizingizio, wamekibatiza “Tume Huru” ili mwisho wa safari wapate huruma ya wasafiri. Oh; chombo hakiko imara, wakati hapo walipo sasa, ni kwa msaada wa chombo hicho.

Ikimpendeza awaulize, ni model hipi itawafaa, wasije wakapata kizingizio, waacheni wachague wenyewe. Pengine wangeipenda ile baba lao la dunia au za ndugu zetu wa Africa, zote kwetu ni kitonga, ushindi kabla ya Angelous. Ile ya baba la baba The Federal Election Commission (FEC) iliyoundwa chini ya sharia iitwayo the Federal Election Campaign Act (1974) inamtaka (POTUS) wao ateue wajumbe sita wakathibitishwe na bunge la Senate. Yaani (POTUT) wetu, ateue wajumbe, awapelekwe kwa Ndungai wakapate idhini yao (CCM >70% members) Waulizeni kama ni hii msiwakatalie wakiitaka.

Au twende na ya Ghana maana ilishabadilisha utawala; iliundwa chini ya sharia iitwayo the Electoral Commission Act (1993). Tena katiba yao Article ile ya 70 (1992, Constitution), Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua wajumbe saba na hao wajumbe saba huunda tume hiyo. Vipi hii imekaeje, jaribuni kuwauliza.

Pengine wangependa tufuate ya jirani zetu, jirani zetu hawa wa Kenya. Wao wana ile yao the Independence Electoral and Boundaries Commission (IBEC). Katiba yao pendwa, ila ya mwaka 2010 inamtaka Rais wao ateuwe makamishina saba na kuhidhinishwa na bunge na tena makamishina hao humteua boss wao (CEO). Ni katika muktadha huu, mintalafu ukweli mtupu; Rais hakwepeki wala haepukiki na anabaki chombo pekee wa kuwahakikishia waungwana uchaguzi ulio huru na wa haki. Period!

 
Period iyo vipi ni ile ya kina dada wanayoingia au ya kuhitimisha? At least iwepo ya danganya toto si hii ya kachukua kaweka waa
 
Hapa kinachotakiwa wabadili kipenhele kinachompa madarakani ya kuteua na kutengua uteuzi muda wowote anaotaka yaani wapewe kinda Kama ilivyo kwa majaji, pili tume iajili watumishi wake wa kudumu hadi ngazi ya wilaya. No nini serikali inang'ang'ania wakurugenzi WA halimashauri kuwa watumishi WA time Kama sio kimajaribio upendeleo kwa nini watu wanaofanya kazi kubwa Kama hiyo wasipewe kinga? Wanaogopa nini,sasa hivi mmekata rufaa ya nini?
 
Huu upupu peleka jahaz asilia waitungie taarabu. Mnaogopa nini kuwepo tume ? Au ndo yaleyale mharifu kuogopa sheria
 
Hapa kinachotakiwa wabadili kipenhele kinachompa madarakani ya kuteua na kutengua uteuzi muda wowote anaotaka yaani wapewe kinda Kama ilivyo kwa majaji, pili tume iajili watumishi wake wa kudumu hadi ngazi ya wilaya. No nini serikali inang'ang'ania wakurugenzi WA halimashauri kuwa watumishi WA time Kama sio kimajaribio upendeleo kwa nini watu wanaofanya kazi kubwa Kama hiyo wasipewe kinga? Wanaogopa nini,sasa hivi mmekata rufaa ya nini?
Mkuu hayo mamlaka yatakua ya ajabu sana yaani yakupe malaka ya kuteua yakunyime kutengua??? Angalia Ghana kwa mfano, 29ThJune, 2018; Rais wa Ghana aliwatimua viongozi watatu waandamizi wa tume huru (refer to: https://www.africanews.com/2018/06/29/ghana-s-president-fires-electoral-commission-head-two-deputies//)

Tena Tanzania haijaanzishisha yenyewe na si ya kwanza duniani kuwa Rais wake ndiye mteuzi wa viongozi waandaminizi wa tume huru ya Uchaguzi: tukiangalia hata huyo anaeitwa baba la demokrasia Marekani hao viongozi wa tume ya uchaguzi wanateuliwa na Rais, hii inafanyika hata katika nchi zinazosifika kwa demokrasia Africa kama vile Ghana na hata jirani zetu Kenya.

Sasa kuna nongwa gani Rais akiteua kama hata linaloitwa baba la demokrasia wanafanya hivyo??? Tena, kwamba tume iajili wafanyakazi MBONA NDIYO INAVYOFANYA! Angalia kwa mfano, kila unapofika wakati wa uchaguzi TUME HUTANGAZA NAFASI MBALIMBALI ZA KAZI watu wanapata temporary jobs nchi nzima. Au ulitaka wawepo viongozi wa NEC kila mtaa/kijiji, kata, jimbo etc KWA WAKATI WOTE?

Watalipwa nini na kwa kazi gani maana uchaguzi si kila siku.
 
Period iyo vipi ni ile ya kina dada wanayoingia au ya kuhitimisha? At least iwepo ya danganya toto si hii ya kachukua kaweka waa
Hii mambo ya danganya toto ndiyo imefanya wanasiasa uchwara wafanye siasa kama biashara...#Tume yetu ipo sawa.
 
Back
Top Bottom