Ati Tanzania walipewa awadi ya Uongozi na Utawala bora kwa maana hiyo iliongoza kwa nchi za kusini..

Ati Tanzania walipewa awadi ya Uongozi na Utawala bora kwa maana hiyo iliongoza kwa nchi za kusini..

Mboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
1,095
Reaction score
293
Nilisoma kwa news kwa gazeti moja hivi siku si nyingi,waliandika hivi Tanzania kinara wa Uongozi na Utawala bora hadi wakatunukiwa cheti cha Utawala na Uongozi bora.
Lakini nikajaribu kuchunguza je hii ni kweli na kama ni kweli hao waliowapa hii tuzo waliangalia vigezo gani hadi kuwatunukia hii tuzo ambayo mie naiona kama ni kubwa atleast.Lakini kusema kweli wandugu sikupata ufumbuzi hadi leo,hivi nikaona hebu nijaribu kupata msaada hapa kwa the Thinkers huenda wakatiririrka nini kilitokea.
Nikija kwa upande wangu mie kama nilivyotaka kuongeza tuzo kwa hii hii habari kusema kweli sijapata hata 5%ya kuweza kuwapatia hawa Watanzania wanaodeal na Utawa wa Sheria kama wanavyojinadi,Tukiangalia majanga ambayo yalipatakina huko nyuma nahata majuzi na mpaka wa leo hakuna tulichosikia juu ya majanga haya ya kuuwa kwa Watanzania ambao hawana hata chembe ya hatia na wauaji wakiwa wanajulikana/wanahisiwa kuwa na uhasama kabla ya vifo hivyo.Tukiangalia suala la juzi tu vifo viwili nachukulia hivi vya juzi lakini tusisahau vipo vya nyuma na sio nyuma kiivyo pia ni hivi karibuni tu.
Tunafahamu sote kuwa sheria ni msumeno yaani unakata nyuma na mbele/kotekote lakini si hivyo kwa Tanzania ambayo imepewa tuzo ya utawala bora hata sifahamu walipewa kwa vigezo vipi kama nilivyoulizia wapendwa hapo juu,cha kusikitisha zaidi ni mauaji ya mwandishi wa habari Daud Mwangosi samahani kwa kurudia hii habari kama kuna wengine washaileta hapa/kama inafanana kwa mbali na hii yangu lakini kusudio langu ni kutaka tu kufahamu kwa undani nini maana ya Utawala wa Sheria.Huyu Ngugu mwandishi wa habari tuliona na kutizama picha na kuona alifia mikononi mwa Polisi tena wakiwa wamemzunguka na mmoja wao kufyatua Bomu na kumuuwa,lakini cha kusikitisha mpaka leo ni mmoja tu wa wauaji ndio kapandishwa mahakamani na wale sita akiwemo Kamanda Kamuhanda wanapiga kazi nakulipwa mishahara yao kama kawa.
Tukija kwa upande mwingine yaani kule Mwanza aliuwawa kamanda yule Liberatus Barlow na mpaka sasa walishakamatwa watu 7 na wameshafikishwa mahakani na hawa ni watuhumiwa nikiwa na maana hawafahamu kama kweli ndio wauaji wa Ndugu Barlow lakini kwa kule Iringa kwa kifo cha ndugu Mwangosi wanajulikana na tuliwaona kwenye picha za video ambazo zipo kwa youtube pia na hata kwa picha za kawaida lakini sheria ile bado inaendelea kukata upande mmoja nikiwa na maana, kwa nini hawa saba wa kusadikika wakamatwe na wale sita wa Iringa ukiondoa 1 ambaye ni keshafikishwa mahakamani hawakukamatwa? na hawa ni Polisi ambao nisememe wanasimamia Uongozi bora na Utawala bora.Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Wewe mwenyewe unaelewa ulichokiandika? nna uhakika wewe ni Mkenya.
 
Back
Top Bottom