JKT Queens yawa gumzo katika fainali hizi, wakiwakilisha kanda ya CECAFA na tayari ma scout wa kimataifa wameshabaini wachezaji wa kuwalenga kuwasajili .
JKT Queens imesheheni vipaji vya wachezaji wa umri wa miaka 15, 16, 17, 18, 19 wanaocheza kikosi cha kwanza (first eleven) ambao wana nafasi ya kucheza soka kwa kipindi kirefu kijacho.
JKT Queens, washiriki wa kwanza kutoka Tanzania, walipata nafasi ya kushiriki michuano hii inayoendelea nchini Cote d’Ivoire kwa kujituma na kujitolea kwa jasho, damu, ukakamavu na hii imeonekana katika mechi mbili ambazo wamecheza hadi sasa ktk champions league group stages inayoendelea .
Safari yao ya ajabu kufikia hatua hii ya kucheza Champions League iliimarika kupitia ushindi mnono wa mikwaju ya penalti dhidi ya timu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia ECB wakati wa mchujo wa kanda wa CECAFA kuwania nafasi ya kushiriki michuano hii mikubwa ya Afrika ya CAF Champios League kwa wanawake.
Kipigo cha leo ngazi ya klabu CAFWCL2023 kinaikumbusha machungu ya mengine waliyotiwa na Tanzania baada ya Twiga Stars kuifunga na kuitoa ktk michuano timu ya taifa ya Wanawake wa Ivory Coast mwezi September 2023 kuwania nafasi ya kucheza fainali za African Cup of Nations mwakani 2024.( Women's AFCON 2024).
Toka maktaba :
TWIGA STARS YAITOA IVORY COAST KWA MATUTA CHAMAZI

TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya mwakani nchini Morocco baada ya kuwatoa Ivory Coast kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya jumla ya 2-2