Atupwa jela miaka 30 kwa kuzaa na bintiye

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Mbeya. Mkazi wa Isanga jijini Mbeya, Yusufu Amani (39) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na Mahakama ya Wilaya ya Mbeya baada ya kupatikana na kosa la kumlawiti, kumpa mimba na kisha kumzalisha mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 15 (jina tunalo).
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa la kumbaka mtoto wake na kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
Alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo huku akijua ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.
Akisoma hukumu hakimu, Gilbert Ndeuro alisema mshtakiwa atafungwa jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia. Alisema anatoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi mahakamani hapo.

MCL
 
kulawiti kisha kumpa mimba au sujui neno kulawiti..yoyote amepata sitahi yake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…