Au Tubadili Rangi

Au Tubadili Rangi

Mr Mhando

Member
Joined
Nov 2, 2018
Posts
17
Reaction score
20
Mlevi na Redio

1

Mlevi kajilaza, chupa mkononi,
Redio inavuma, kwa sauti laini,
Sifa kwa rangi, zinasikika mbali,
Lakini mitaani, shida ni ile ile.

2

Barabara mashimo, taa hazing’ai,
Bei ya chakula, imeshika mbio,
Ajira ni ndoto, vijana wanalia,
Lakini wasema, "Maisha ni bora!"

3

Mlevi kacheka, macho yakimwaga,
"Acheni mchezo, acheni mizaha,
Mmekula vyote, mkabaki na sifa,
Na sisi tunakosa hata ya asubuhi!"

4

Akapiga funda, akafikiri sana,
"Labda tubadili njia na mawazo,
Labda twende mbele kwa mwendo mp
ya,
Au tubadilishe rangi!"
 
ngoja ninywe kidogo labda nitamwelewa mlevi
 
Back
Top Bottom