Aua mke mjamzito kwa kipigo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Adaiwa kumuua mkewe siku chache baada ya ndoa

Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumuua mkewe mjamzito aliyefunga naye ndoa siku chache zilizopita.

George Marito mwenye umri wa miaka 28 anadaiwa kutenda kosa hilo Jumapili iliyopita ambapo alimpiga Dorcas Nyaboke hadi kufa kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi na mashuhuda baada ya kutekeleza tukio hilo alijaribu kujiua kwa kujirusha kwenye maporomoko ya mto Kegati lakini kuna mpita njia aliyemuona baadaye akamuokoa na kumrudisha nyumbani kwake.

“Baada ya kumfikisha nyumbani, yule jirani yetu alishtuka kuona mwili wa Nyaboke ukiwa umelala sakafuni, pembeni kuna matapishi,” jirani aliyejitambulisha kwa jina la Isaboke alizungumzia tukio hilo.

Uchunguzi wa awali wa polisi umeeleza kuwa Marito alirejea nyumbani kwake Jumapili usiku majira ya saa nne, na alipoulizwa na mkewe sababu za kurejea usiku huo kwani amechelewa walitofautiana kauli na ndipo alipoanza kumpiga.
 
Ndoa za Wakenya ni kuuana tuuu shida ni nini jirani zetu?
Kila mwezi 'mume kaua mke' mchepuko kaua mke mke kaua mume nini shida wajameni?
Sisi huku sio kama hayapo, yapo lakini wenzetu mmezidi kha!
 
Hao wakenya SI wanapigwaga na wake zao

Leo vice versa.[emoji3][emoji3]
 
Ndoa za Wakenya ni kuuana tuuu shida ni nini jirani zetu?
Kila mwezi 'mume kaua mke' mchepuko kaua mke mke kaua mume nini shida wajameni?
Sisi huku sio kama hayapo, yapo lakini wenzetu mmezidi kha!
Anikwa kile kipindi ni cha kipumbavu sana!
 
Mmoja wao lazima itakuwa alikuwa anasema sana.Hasira zinapokuwa juu na kama unajua mwenzako anasema sana,ni afadhali utoke nje ukae nae mbali kwa muda wa hata masaa 2,ili apoe kwa maana kuna watu wakianza kuongea hawana break,kashfa,kejeli wakati anajua kabisa kuwa nguvu hana...
 
Hii n aibu kwa taifa la kenya alafu yaan hapa ndio kwa ku prove wrong wale waliobdai tz inashikannafasi ya 3 kwa stress ...taifa kamamla kenya linapaswa kiwe la kwanza kwa stress na kuuana
 
Ndoa za Wakenya ni kuuana tuuu shida ni nini jirani zetu?
Kila mwezi 'mume kaua mke' mchepuko kaua mke mke kaua mume nini shida wajameni?
Sisi huku sio kama hayapo, yapo lakini wenzetu mmezidi kha!

Mapenzi ugonjwa hatari sana. Duh...
 
Mkuu wengine huwa hawapoi,,, ukirudi tu ni kama umeng'oa koki anatiririka tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…