Audio: Msikilize Jide akithibitisha rasmi kuwa Amemuacha Gadner

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe
kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G
Habash imevunjika.
Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha
Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye
uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya
kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa
akiteswa.
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa
siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi
kwenye vyombo vya habari.
“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu
ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye
media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote
ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha
yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote
wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu
anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee
kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na
privacy. Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza
kuelezea mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au
mume wake alimfanya hivi, sidhani kama kuna mtu yeyote
anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele za
watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja
wa watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili.
“Swali nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil
Haule, mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”
Isikilize interview hiyo hapo chini.
Credit Bongo5
Lady Jaydee: Nimemuacha Gadner (Audio) – Bongo5.com

Audio: Lady Jaydee kuhusu Gadner by Bongofive - HulkShare
 
aendelee kupiga kazi tu......... na lep 28th tukasapoti kazi

za mikono yake pale MOG.

MWnaume malaya kuacha umalaya ni kazi sana

Hahahaha kwahiyo pale MOG kunaendeshwa na hela za MKONO aliyekula fedha za shirika la Umeme Tanesco?
 
Sasa huyo bibi atapata mwanaume kweli na viguu vile vya bata?litakua ajabu la nane la dunia
 
Duuuu. Haya mwanamke! Lakini nikushauri kitu unaposema umemuacha sijui wewe unapata amani kiasi gani? Kwanini usitumie neno tumeachana uendelee kuhifadhi hayo mahusiano yenu ya awali ili usitengeneze maswali wala mashindano. Pia itakusaidia kusonga mbele bila kinyago ndani ya moyo wako. Kusamehe kunaleta amani ya kweli.

Lakini inawezekana yeye alishakuacha siku nyingi na haukua moyoni mwake ilibaki kwake kuchukua hatua na ukute alijua ili isiwe tabu akianza yeye akaona akusukume ili mwenyewe utamke aendelee na business zake. Hayo ndio mambo ya moyoni haiwezekani anakupenda, uko moyoni akupige hadi kukutoa alama au akunyanyase hali wewe umemuhifadhi.

Kingine utubu na umshukuru Mungu kakupa second chance ulichokifanya hakikuwa sahihi. Mwaka uliofunga hiyo ndoa ulimake headlines kwa kuonyesha kuwa wewe ni kiboko wa kunyoosha mume wa mwenzio hata ilifikia mahali ilionekana una uwezo wa kulea mtoto wake wa ndoa( ulee baba na mtoto) ningeshangaa yule dada angekupa yule mtoto! Walioelewa maana hasa ya ndoa walikushangaa sana but mwenye nafuu mpishe ukang'ang'ana bi dada ukafunga ndoa heka heka! Kiko wapi mfupa uliomshinda fisi. ......! Lakini ndio vizuri na hope umejifunza kitu, through that experience ikusaidie kusaidia wengine watakaotaka kukosea kama ww.

Na zaidi uwe unajifunza kwa makosa ya wengine yaliyopita usitake kujifunza kupitia makosa yako utaumia na kuendelea kupoteza muda.

Mwisho kama yanayoongelewa ni sahihi shost ulishaachwa siku nyingi na si dhambi. Kubali matokeo songa mbele usiendelee kupoteza muda. Ninajua wewe ni kioo cha jamii hili ilikua lazima siku moja ulizungumze jitahidi kutumia sentesi ambazo hazina ukakasi, na uelewe maisha ya mashindano yana gharama. Na penye vurugu Mungu hakai hapo.

Achana naye aende zake Mungu atakusaidia.

Pia ujue si wanaume wote wanastahili kuwa waume jide kama ambavyo si wanawake wote wanaokuwa wake!

Yangu mimi hayo tu
 
Yaani marioo umlishe umvishe na hela ya kuhonga machangudoa umpe halafu akupige. Shwetani kabisa huyo mariooo gardner.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…