Audio iliyopachikwa hapo ni ya kipindi cha Njia Panda kilichorushwa na redio Clouds FM kila siku za Jumapili.
Kipindi kilichorushwa hewani tarehe 27 Machi 2011, kilihusu "uponyaji" unaotamkwa kuwa unapatikana Loliondo....
Mahojiano katika kipindi hico kiliwashirikisha wataalamu wa Afya, Mmoja wa wagonjwa aliyekunywa dawa na kudai anajisikia kupona na Wachungaji wawili wa madhehebu tofauti ya Kikristo.
Mwendesha kipindi ni Dk. Isaac Maro.
NB: Kipindi kimewekwa vivyo kilivyorushwa, hakuna uhariri wowote uliyofanyika ili upate picha kamili ya kilichojiri siku hiyo.