Audio/video ya hotuba ya Jaji Mstaafu Warioba ktk Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba

Audio/video ya hotuba ya Jaji Mstaafu Warioba ktk Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba

MAN OF CHANGES

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2011
Posts
507
Reaction score
191
Jana mzee huyu ameweka historia mpya ktk taifa letu,amejibu maswali mengi sana ambayo kwa vizazi vijavyo watakuja kutuuliza.Tafadhali mwenye link ya kutuwezesha kupata audio/video ya hotuba yake ya jana atuwekee hapa,tupate kumbukumbu hiyo muhimu sana kwa taifa na historia ya taaifa letu.
 
Nimemsikiliza huyu mzee na sijaamini kuona pamoja na umri wake ameweza kusoma hotuba ndefu kwa umahiri na kaangusha nondo nzito sana
 
Sema kaangusha upuuzi!! Maana ndiyo msimamo wa chama chako,, ikiziita nondo unaweza kutimuliwa chamani.

Mpaka sasa hivi sijaona mfuasi yeyeto wa CCM akimuungu mkono ndugu Chris Lukosi kwa sababu sio msimamo wa chama chao vijana wanarubuniwa na uchama na kusahau utaifa kuwa hivi vyama CCM na CHADEMA, NCCR, CUF, ACT kuna siku vitakufa ila katiba ya nchi itabaki
 
Last edited by a moderator:
Mpaka sasa hivi sijaona mfuasi yeyeto wa CCM akimuungu mkono ndugu Chris Lukosi kwa sababu sio msimamo wa chama chao vijana wanarubuniwa na uchama na kusahau utaifa kuwa hivi vyama CCM na CHADEMA, NCCR, CUF, ACT kuna siku vitakufa ila katiba ya nchi itabaki
Mimi napigania future ya wanangu...

Hii katiba inaandaliwa kwa ajili yetu sote bila kujali vyama.
 
Dira la taifa, seriously someone should have handed this old man and his entire team politics 101 handout. Hakuna mtu asietaka kuona maisha ya watu yanaboreshwa au huduma bora na zenye viwango zina mfikia kila mtu, swala ni jinsi ya kuzigharamia hizo huduma na kuwa na budget yenye huwezo huo.

Tafsiri yenyewe ya siasa, inasema lengo la siasa ni kujaribu kutimiza matakwa ya wengi au kuja na mbinu zenye faida kwa wengi. Sasa tukianza kuangalia demand za individuals na kujaribu kuzitimiza bila ya kuzingatia huwezo wa mfuko wa taifa hizo zinakuwa ni hadithi na kibaya zaidi unapomwambia mwanakijiji swala hilo litafanyiwa kazi bila ya kumpa ukweli wa mambo ni kumpotosha. Hivi vitu haviwezi kuwa kwenye katiba, kwa maana ukiviweka ni tayari umeweka mkataba na bench mark ambayo auna uhakika wa kutimiza, ndio maana wanasiasa wantakiwa kuchuana kwa hoja na jinsi gani wanaweza fikisha malengo fulani fulani ya makundi kwa sababu hivi vitu vinataka uelewa wa uchumi, hali halisi ya maisha, population na uwezo wa kifedha. Sasa mtu anaweza vipi kusema mkataba utoe kiwango fulani cha huduma, aseme na hela itatoka wapi kwanza hizo variables za taifa hazipo constant year to year and could easily be influenced by global events kwa kweli hawa watu sijui walikuwa wanafikiria nini.

Kikomo cha ubunge na mawaziri kutokuwa wabunge, si kwamba zana nzima ya demokrasia wali isahau bali hata issue za checks zinampiga chenga seriously this old man sometime in the past was prime minister and jaji mkuu on merit au anawabeza tu wenzake? Mbona anapwaya sana kwenye misingi rahisi sana kuitolea ufafanuzi na wala sikumtukana. Hivi waziri kuwa mmbunge au kutokuwa mmbunge what is the difference, iwapo bunge ni sehemu ya checks za serikali and where ministerial (or executive branch) policies are scrutinized and debated. Bunge litawezaje kusikia testimony za serikali hiwapo waziri aingii bungeni kuelezea sera zimetokea wapi au kuelezea faida zake, si wabunge watajiamulia tu au itakuwa kujibizana na media i dont think that is the best way to scrutinize the government policies. Vilevile raisi hawezi kuchagua mtu tu kuwa waziri lazima awe anaelewa ilani ya chama chao kama waziri na katibu mkuu yupo kwenye wizara kwa sababu ya kulenga kile serikali imekipanga.

Sasa unapotaka mmbunge asiwe waziri au raisi achague mawaziri kwa mtindo mwengine, wakati wao wameingia madarakani kwa ahadi walizotoa halafu unamwambia asitumie timu yake sijui unakiweka chama chochote cha siasa katika giza nene sana. Yaani kuna mambo mengi sana huyu babu kajianzia tu, tume ya taifa kuchunguza maadili ya wafanyakaza wa serikali, tatizo letu tunafanya vitu kwa ku-copy tu miundo ya wenzetu, jamaa wakisema kazi ya bunge ni kufanya checks za serikali hawatanii, kwa sababu waziri akishatoka bungeni, kazi za kamati ya bunge zinaingia kujua sera itafikia wapi kwa kina, idadi ya watakao faidika na kuifanyia sera 'baseline assessment' or 'summative assessment', kujua wizara imejipangaje, kuchunguza tenda zinazotolewa, matumizi ya hela na mambo mengi.

Tatizo letu sisi tuna misingi lakini hatujui inafanya kazi vipi kwa hivyo tatizo sio njia za checks bali uwezo na ufahamu wa watu wanaotakiwa kufanya checks, mweh this man was supposed to produce a panacea what we are getting is worst than what we had mpaka nilipofikia kwa maoni yangu, waziri kupendelea kwao kamati ya bunge kwanini wasiulize wizara husika kujenga ofisi za bunge uramboni au barabara sehemu fulani ilikuwa ni kwasababu za kimkakati, au imekuaje Mwanga juu kuna umeme wakati huku upareni chini jamaa wameacha kuweka mitambo hapo sidhani kama tatizo kwa sababu ya mtu kuwa mmbunge waziri/tatizo ni wanaotakiwa kukosoa sera na mwenendo wa matumizi ya serikali.
 
Back
Top Bottom