kevylameck
Member
- Nov 3, 2013
- 18
- 19
Baada ya miaka 10 kupita,Sensa ya watu na makazi ya mwaka huu itakuwa ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Sensa nyingine kulingana na Sheria ya Takwimu Sura 351 kifungu kidogo cha 6(2)(a) zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na August 2012.
Sensa ni zoezi la kupata idadi ya watu wote nchini, kwa umri na jinsi, mahali wanapoishi, viwango vyao vya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo, hali ya makazi na taarifa nyingine nyingi muhimu.
Zoezi la sensa hufanyika kwa kutumia karani wa sensa kwenye eneo la kijiografia ili kuhesabu kaya na watu wote waliolala kwenye kaya husika usiku wa kuamkia siku ya sensa pamoja na kuchukua taarifa zao kulingana na maswali yaliyopo kwenye dodoso.
Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu, anasema takwimu sahihi kuhusiana na watu ambazo zimechambuliwa na kuainishwa kwa makundi, ukubwa na mtawanyiko wa watu na makazi ni muhimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo
Takwimu na taarifa zitakazokusanywa zitatumika baadae kupanga na kutunga sera za kiuchumi, kijamii na mazingira na pia kutathmini ubora wa hali ya maisha ya watanzania kwa ujumla.
Kulingana na Katibu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Kenani Kihongosi, anasema serikali inatambua kuwa ni vigumu kupata maendeleo endelevu bila kuwa na takwimu sahihi na za kuaminika kuhusu watu wake pamoja na makazi yao.
Katika Kampeni zake, Kenani Kihongosi anasema ni wajibu wa kila Mtanzania kujiandaa na kushiriki na kutimiza wajibu wake kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.
Karibu August! Karibu mwezi wa kuhesabiwa! Mimi nimejiandaa na nipo tayari kuhesabiwa. Wewe je?
#Ushirikiwakonimuhimu
#Sensakwamaendeleo
#Sensainaharakishamaendeleo