Mateso
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 259
- 19
YES. Nakumbuka Mwalimu siku moja alikuwa akizungumza na waandishi wa habari 1995 akasema ili kuwepo na upinzani wa kweli lazima mtu atoke ndani ya CCM. Hivyo akamshauri Mrema ahamie NCCR baada ya kuzungumza na kina Marando. Kwenye uchaguzi mkuu wa 1995 Mrema akatangaza lengo lake la kugombea urais kupitia NCCR. Mwalimu akamwita akamwambia akagombee ubunge aachane na urais Mrema akamkatalia tena akazungumza hadharani akasema ''Nyerere huyo huyo aliyeniambia niondoke CCM niende upinzani ni Nyerere huyo huyo anayeniambia nisigombee urais nigombee ubunge.'' Sasa hapa utajua wazi kuwa Mrema amewekwa kama mvurugaji wa upinzani. Ndo maana anawashawishi wenzake waungane na wakishaungana ikikaribia uchaguzi anawavuruga wote wanagombana mara CCM inashinda. Huyu ni ndumila kuwili hafai kabisa.