Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!


Kuungana ni wazo zuri sana, ila tatizo kuna vyama pandikizi, hivi hata mkiungana vitawavuruga zaidi. Niliwahi kuanzisha thread ambamo nilizungumzia Sitta kubaki CCM lakini afanye kazi ya upinzani; kama vile CCM inavyopandikiza vyama au wanachama/viongozi katika upinzani ili ipate siri zake na kuwavuruga kirahisi. Ebu kumbuka mgombea urais (toka upinzani) wa mwaka 2005 ambaye sasa amerudi CCM! Ni hatari, mnaweza kuungana na mkamuweka mgombea mmoja lakini karibu na mwisho wa kampeni anatangaza kurudi CCM; linakuwa ni pigo tosha!
Sisi wenyewe tumeshapambanua mpinzani wa kweli ni yupi, basi tumuunge mkono huyo huyo, hao wanaobaki wataamua wenyewe kuungana naye au kubaki walivyo!
 
Huo ulioutaja ni ushujaa wa kwanza - kujitoa CCM
Pili kumbuka alivyokamata dhahabu ya wakubwa pale airport (na hapa ndipo alianza kutofautiana nao).
Tatu, kumbuka alivyowasema waziwazi akina patel na mashamba ya mkonge - ni wale wale patel wa sasa! mpaka mzee wa Tanganyika akawaita ma*********
Kumbuka watu walivyosalimisha silaha katika vita dhidi ya ujambazi na namna alivyoendeleza mkakati wa sungusungu
the list is very long.
Hata Nyerere alikuwa anapiga kampeni akisema mchagueni Mkapa lakini hakuna mahali popote aliposema Mrema ni mbaya!
Kuanguka kwake katika NCCR Mageuzi ni akina Mabere ambao aliamini ni wapinzani wa kweli kumbe wapi; inasemekana walitaka hata kumuua mkutanoni Tanga kama si mlinzi wake kumkata mtama akaanguka na risasi ikapita!
Historia itamtaja kama shujaa kweli. Ngoja CCM ianguke uone ukweli uakavyojulikana!
Yuko wapi tuliyemuona kuwa shujaa wetu pale manzese na Ubungo Dr. Lamwai, si amejionyesha asivyokuwa shujaa! hao ndio walimdanganya mrema. Yuko wapi makongoro nyerere, si alirudi ccm - ni katika kundi lililokuwa na mrema nk. Nakubalina na aliyesema kuwa mrema aliamini kuwa kila aliyeko upinzani ni mpinzani wakweli kumbe wapi - wengine walikuwa ni vibaraka wa CCM kama ilivyojidhihirisha baadae.
Na hili ndilo linafanya muungano wa wapinzani usiwezekane maana unamuona leo ni mpinzani kesho anarudi CCM. Mrema ana udhaifu wake kama mtu lakini kwa upinzani ni mpinzani kweli maana hata akianza kuhutubia utaona alivyojawa na uchungu na nchi hii - akionyesha hivyo watu wanaambiwa eti ana jazba - siyo jazba, ni uchungu na uzalendo! Please...!
 

Hapana asingekuwa president kwanza Nyerere hakuwa amemuweka katika msururu wa aliokuwa amewaandaa, pili tayari kwa utendaji wake alishtofautiana na wakubwa (kukamata dhahabu airport, utapeli katika uwekezaji katika mashamba ya mkonge nk), hivyo asingeweza kupita katika NEC.
OK. Mrema hatakuwa rais lakini kujitoa kwake ccm kuliwafumbua macho wananchi na kuanza kuona kuwa upinzani ni jambo zuri. Kumbuka wakati wa kura za maoni kama vyama vingi vianzishwe au la, asilimia 20 tu ndio walisema vianze, lakini mrema alipotoka CCM, katika uchaguzi alipata around 40% Wonderful! - Na hii ni baada ya kuibiwa kura nyingi sana - kumbuka DSM majimbo yote wapinzani walikuwa wameshinda - saa nane usiku ikatangazwa kuwa uchaguzi wa DSM tu umefutwa! au mmesahau?
 
Tafuta yaliyotokea katika mkutano wa NCCR mageuzi Tanga ndipo utaona utapeli wa akina marando na si mrema. Wakati mrema anasema tukakiuze chama kwa wananchi hadi chini kabisa, marando akasema hatuhitaji chama kikubwa namna hiyo! (then hicho kisingekuwa chama, labda pressure group)
Sisi wenyewe ndio tulimwambia toka huko maana hao hawana dhamira ya kweli ya upinzani, ndipo akatafuta chama kilichokuwa kidoogo sana TLP akajiunga nacho kwani asingeweza kuanzisha chake (wangemzengwe) na pia hiyo ingeongeza utitiri wa vyama.
 
Kamakabuzi,

..sasa alipofika TLP kwanini hakujenga chama toka chini kama alivyokuwa amedhamiria kwa NCCR?

..mimi nadhani Mrema ana mapungufu makubwa kwamba hawezi kufanya kazi vizuri na viongozi wenzake.

..karibu kila chama alichokwenda amekuwa mtu wa vituko-vituko tu.

..nadhani hata CCM wangempa madaraka Mrema leo hii wangekuwa wamesambaratika.
 
Labda nitakuwa na upungufu wa misamihati lakini nadhani Mrema alikuwa na Guts. Neno shujaa ni lazima liambatane na busara, strategies za kushinda au kufikisha ujumbe vitu ambavyo viko kwenye short supply tukimzungumzia ndugu Mrema.

.

- Mkuu Zakumi, heshima mbele sana, maana hapa tupo ukurasa mmoja.

Respect.

FMEs!
 
Kweli amekuwa mtu exeptional pamoja na kwamba tulimwazia tofauti, hakuna aliye kamili lakini yale mazuri zaidi yanapoonekana hatuna budi kuyasema. Mrema amekuwa mpinzani mahiri wa kwanza Tanzania, tukiachana na mabaya yaliyomtokea, ukweli utabaki kwamba alikuwa mzalendo wa ukweli na hata Mwalimu angeibuka leo hii angemwambia mwanangu shika hili rungu hawa wangu walikuwa wanafiki nikiwa hai.


An innocent person never dies in his own house
 
Kweli amekuwa mtu exeptional pamoja na kwamba tulimwazia tofauti, hakuna aliye kamili lakini yale mazuri zaidi yanapoonekana hatuna budi kuyasema. Mrema amekuwa mpinzani mahiri wa kwanza Tanzania, tukiachana na mabaya yaliyomtokea, ukweli utabaki kwamba alikuwa mzalendo wa ukweli na hata Mwalimu angeibuka leo hii angemwambia mwanangu shika hili rungu hawa wangu walikuwa wanafiki nikiwa hai.

An innocent person never die in his own house
 
Zakumi,

..by the time Mrema anakwenda upinzani, serikali ya CCM ilikuwa very unpopular.

..kulikuwa na migomo karibu ktk kila taasisi kuanzia waalimu, madaktari,wanafunzi chuo kikuu, na hata wanajeshi inasemekana walikuwa very frustrated.

..kwa msingi huo kujitoa ktk serikali ambayo tayari imekosa umaarufu na imepoteza uhalali machoni mwa wananchi sidhani kama ni tendo la kishujaa, au kuwa na guts hata kidogo.

..Mrema alikuwa humohumo akiuma na kupuliza, akiwatikisa wana CCM wenzake ili apate ulaji zaidi--kumbuka alivyokamata dhahabu na kuishia kuwa Naibu Waziri Mkuu, sasa mwisho walipokosana ktk ulaji/mgao ndiyo akaamua kujitoa.

..Mrema alikuwa maarufu kushughulikia matatizo ya wizara nyingine wakati wizarani kwake mambo ya ndani kumedorora.

..katika kipindi chake cha uwaziri wa mambo ya ndani usafirishaji madawa ya kulevya ulikithiri nchini. utoroshwaji wa nyara za serikali kupitia viwanja vya ndege na bandarini uliongezeka kwa kiwango kikubwa. noti bandia zilisambaa nchi nzima. uingizwaji bidhaa za magendo mipakani, na kwa kiwango kikubwa kupitia ktk jimbo lake la uchaguzi, ulikithiri.
 

Kabla ya kuendelea itabidi niweke sawa. Mkwawa alikuwa na strategic nyingi sana zikionyesha umakini wake kama kiongozi. Kwanza alikuwa na vikosi vya wapepelezi, vilivyompa taarifa ya maendeleo ya wajerumani na kuweza kuandaa majeshi yake.

Pili aliweza kupigana ana kwa ana na kushinda vita ya kwanza. Aliposhindwa vita ya pili alianza Guerrilla warfare iliyochukua zaidi ya miaka mingi.

Commit suicide kulitokana na ukweli kuwa alikuwa THE LAST SOLDIER STANDING. Characteristcs za Mkwawa hazipatikani kwa viongozi wetu wa sasa.

Tukirudi kwenye mada. Ni lazima yawepo maelezo ya nani mpiganaji. Mpiganaji ni mtu anayepigania kitu (Rebel With A Cause). Hama sivyo upiganaji utakuwa fashion statement kama tunavyoona sasa.

Mrema kwa kutokuwa na mipangilio alilipotezea taifa muda tu.
 
Mkwawa alikuwa na strategic nyingi sana zikionyesha umakini wake kama kiongozi. Kwanza alikuwa na vikosi vya wapepelezi, vilivyompa taarifa ya maendeleo ya wajerumani na kuweza kuandaa majeshi yake.

There you sound like the socialist Companero...Lol
 
 
Mrema bwana anajijua mwenyewe hata haeleweki...uchaga umemjaa sana. Mi nafikiri tuwe wa kweli maana mrema hakuna anachokifanya zaidi ya kuota urais ndo maana chama chake hakijafika popote kisa majungu yake ya kung'ang'ania cheo kikubwa. Hana tofauti na Mbowe
 


Jokakuu:

Nashukuru kwa kunipa elimu nzuri kuhusu Ndugu Mrema. Nilikuwa mshabiki sana wa Mrema wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995. Aliposhindwa kwenye uchaguzi huo nilikata tamaa na siasa za Tanzania na kwa zaidi ya miaka miwili niliachana na debates za siasa.

Lakini miaka ilivyoendelea baada ya uchaguzi niliona kuwa ana kasoro za namna fulani ambazo zilifanya yeye kuwa ni tatizo na sio solution.
 
Zakumi,

..binafsi nilikuwa NCCR lakini Mrema alivyokwenda huko nikakosa imani na chama kile.

..kama ulivyoelekeza mwanzoni, kwamba bila kuwepo mfumo thabiti wa checks and balance, basi tutaendelea na huu mduara wa ufisadi milele na milele.

..mfumo wetu wa sheria na checks and balance ni so weak kiasi kwamba kiongozi wa Tanzania kutokushiriki ktk ufisadi ni kama suala la hiari au opptional.

..sasa ndio maana unakuta viongozi wanaingia madarakani wakiwa wasafi, na wanazungumza kwa ukali dhidi ya rushwa, lakini baadaye wanaona mazingira yanawaruhusu na wao kushiriki ufisadi kwa hiyo wanatumbukia humo.
 
 

Na mpaka sasa juhudi za nchi ni kutafuta the next Nyerere, mtu ambaye si fisadi kwa hiari. Zoezi hili ni matokeo ya bahati nasibu. Cha muhimu ni checks and balance na zaidi tuwe transparency katika shughuli ya umma.
 

Mrema ana matatizo yake lakini sioni kama yanaingiliana na kabila lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…