Aunty Ezekiel: Eeh Mungu nisidie nijifungue salama

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Msanii wa filamu Aunt Ezekiel ambaye hivi sasa ametibuka kutokana na ujauzito mkubwa alionao, ameeleza kuwa kila saa na kila siku anamuomba Mungu amjaalie ajifungue salama maana maneno ya watu yamekuwa yakimtisha.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Aunt alisema kuna watu ambao wamekuwa wakimuombea mabaya kutokana na chuki zao lakini yeye anaamini Mungu ndiye kila kitu kwake.

"Wapo watu ambao wanaisengenya mimba yangu, wananisema vibaya, wananiombea mabaya kiasi cha kunipa hofu. Lakini yote kwa yote namuomba Mungu nijifungue salama," alisema Aunt.
 
Leo usipozaa basi huzai tena
 
Uzae salama bibie Anti kwa kuamua kuwa na mtoto all the best kwenye kuleta kiumbe duniani Mungu akupiganie.
 
Anajishtukia tu nae ye ajifungue tu
 
Uzae salama bibie Anti kwa kuamua kuwa na mtoto all the best kwenye kuleta kiumbe duniani Mungu akupiganie.

Si nimewahi kusikia kua aliwahi kuzaa mtoto akafa? Au mimba iliharibika?Sikumbuki vizuri.
 
Si nimewahi kusikia kua aliwahi kuzaa mtoto akafa? Au mimba iliharibika?Sikumbuki vizuri.

Nilimuona akihojiwa na Mkasi akasema kipindi hicho alikua na Jack Pemba wakati wa ujauzito akampiga mimba ikaharibika ila nampa hongera Bongo movie hawataki kuzaa wanaona soko litapungua.
 
Nilimuona akihojiwa na Mkasi akasema kipindi hicho alikua na Jack Pemba wakati wa ujauzito akampiga mimba ikaharibika ila nampa hongera Bongo movie hawataki kuzaa wanaona soko litapungua.

Wanaogopa kipindi cha ujauzito watakosa madanga.Mbona uwoya na batuli wamezaa lakini bado wazuri tu?
 
Wanaogopa kipindi cha ujauzito watakosa madanga.Mbona uwoya na batuli wamezaa lakini bado wazuri tu?

Ndo wanavofikiria kuchuna kutapungua ndo mana Zari anaheshimika pamoja na watoto bado mzuri hata kina Uwoya akina pangu kauka tia mchuzi hawana ubavu.
 
Tunakuombea mwaya mungu atakusaidia utajifungua salama na utapata mtoto mwenye afya tele.
 
Wanaogopa kipindi cha ujauzito watakosa madanga.Mbona uwoya na batuli wamezaa lakini bado wazuri tu?

Irene mzuri nyie nilimuona jana mhh hatar ila kapungua tu
 
Si nimewahi kusikia kua aliwahi kuzaa mtoto akafa? Au mimba iliharibika?Sikumbuki vizuri.

Jack pemba eti alimpiga mpaka mimba ikatoka, alipat miscarriage, mi nais itakuwa induced abortion tu, maana alivyokuwa akiongea na alivyo usoni unajua kabisa uongo, haonyeshi ata kuumia mxiuuu
 
Wanaogopa kipindi cha ujauzito watakosa madanga.Mbona uwoya na batuli wamezaa lakini bado wazuri tu?

Ye waswas umemjaa tu af nlidhan keshazaaga na mabetto nae keshajifungua mimba aliificha hatare
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…