Australia: Maelfu ya watalii waamriwa kuondoa kutoka maeneo yaliyoshambuliwa kwa moto

Australia: Maelfu ya watalii waamriwa kuondoa kutoka maeneo yaliyoshambuliwa kwa moto

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Maelfu ya watalii wameamriwa kuondoka kutoka maeneo yaliyokumbwa na janga la moto nchini Australia wakati taifa hilo likijitayarisha kwa wimbi la joto kali linalotarajiwa kuongeza kasi ya kusambaa kwa moto unaendelea kuwaka.

Moto mkubwa ulioyashambulia maeneo ya kusini mashariki ya nchi hiyo wakati wa mkesha wa mwaka mpya umesababsiha vifo vya watu nane huku maelfu ya watalii wakikwama kwenye miji ya pwani kutokana na kusambaa kwa moshi.

Watu wanaouzuru maeneo hayo wameonywa kuwa wanapaswa kuondoka kabla ya Jumamosi siku ambayo inatabiriwa kutakuwa na upepo mkali pamoja na kiwango cha joto kitapanda kufikia nyuzi 40.

Hali hiyo ya hewa inaongeza kitisho cha kusambaa kwa moto unaondelea kuwaka na maafisa wamesema hali inaweza kuwa mbaya kuliko ile iliyotokea siku Jumanne.
 
Back
Top Bottom