#COVID19 Austria yaondoa vizuizi vya Corona kwa waliochanjwa

#COVID19 Austria yaondoa vizuizi vya Corona kwa waliochanjwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Austria imeondoa leo vizuizi kwa watu waliopata chanjo kote nchini humo, wiki tatu baada ya kutangaza upya masharti makali ya kupambana na kupanda kwa wimbi la maambukizi ya virusi vya corona.

Masharti hayo, ambayo yanatofautiana na kila jimbo nchini humo, kwa kiasi kikubwa yanaruhusu kufunguliwa tena leo kwa kumbi za sinema, majumba ya makumbusho na maeneo mengine ya utamaduni na burudani.

Maduka yatafunguliwa kesho. Watu ambao hawajachanjwa wataendelea kuwekewa vizuizi na watabakia majumbani isipokuwa tu kama ni sababu za msingi kama kwenda kununua chakula, kumuona daktari au kufanya mazoezi.

Nchini Ujerumani waandamanaji wamekabiliana na polisi dhidi ya vizuizi vya corona katika miji kadhaa. Kulikuwa pia na maandamano kama hayo katika miji ya Instabul na Ankara nchini Uturuki.
 
Back
Top Bottom