Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Baadhi ya magari siku hizi, hususan yenye automatic transmission, yana hii teknolojia inayoitwa automatic start/stop technology.
Kwa ufupi iko hivi;
Gari inakuwa na smart key. Hii smart key ndo unayoweza kuitumia kufungulia milango ya gari, trunk, na kadhalika.
Unaweza ukabonyeza vitufe vilivyopo kwenye smart key au unaweza tu kuiweka mfukoni na ukiwa karibu na gari, unaweza kufungua milango kwa kubonyeza vitufe vilivyopo kwenye handles.
Ndani gari linakuwa halina sehemu ya kuingiza ufunguo.
Badala yake kunakuwepo kitufe ambacho unakibofya na gari inawaka.
Sasa ukiwa unaendesha halafu ukafika sehemu ukasimamisha gari, mfano kwenye taa, injini inajizima kiaina.
Ukitoa mguu kwenye breki, injini inajiwasha tena.
Hii pia hutokea ukiwa kwenye foleni kubwa. Foleni ikiwa inaenda taratibu sana, kuna muda unalazimika kufunga breki na kusimama kwa sekunde kadhaa kabla hujasogea tena.
Lengo la hii teknolojia ni kupunguza matumizi ya mafuta na kupungiza emissions.
Sina uhakika sana na ufanisi wake. Ila ninachoweza kusema ni kwamba, ukiwa kwenye eneo/ sehemu ambayo ina tatizo la msongamano mkubwa wa magari barabarani, inakera sana gari kujizima na kujiwasha yenyewe kila mara.
Nani mwingine ana tajiriba na hii teknolojia? Vipi mtazamo wako? Yay or nay?