SheriaE
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 606
- 447
KENYA: Avamiwa na Siafu baada ya kukataa kuoa binti ya mganga
Kijana aliyekodi nyumba ya kifahari ya mganga eneo la Kiritiri kaunti ya Embu nchini Kenya alilazimika kuhama alipovamiwa na siafu baada ya kukataa kuoa binti wa mpiga ramli huyo. Inaaminika kuwa tangu alipohamia katika nyumba hiyo, mpiga ramli huyo amekuwa akimshawishi amuoe binti yake, kwa ahadi kuwa kama akifanya hivyo, atampa jumba lake hilo la kifahari.
Hata hivyo, kijana huyo alimwambia mganga kwamba hawezi kumuoa bintiye kwa kuwa hampendi. Inaelekea hilo lilimuudhi mganga huyo kwani siku moja kijana alipokuwa amelala usiku alivamiwa na siafu, na hivyo kumbidi kuhama nyumba hiyo.
Source: CRI Kiswahili