Aveva amvuta Mbuyu Twite klabu ya Simba

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva yupo kwenye mazungumzo na kiungo mkabaji aliyemaliza mkataba wa kuitumikia Yanga rai wa DR Congo Mbuyu Twite, ili kumsajili kwa ajili ya kuwaongezea nguvu kwenye mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom unaotarajiwa kuanza Desemba 17.

Aveva amesema , wanamuhitaji Twite, kutokana na uwezo aliokuwa nao na wanaamini atawasaidia kwa siku za karibuni kabla ya mchezaji huyo kuamua kustaafu.

“Nikweli tupo kwenye mazungumzo na Twite, bado hatujaafikiana baadhi ya mambo kingine kilichochelewesha tulikuwa tunamsubiri kocha ili aweze kuidhinisha usajili wake ambao kama utafanikiwa atatusaidia kucheza kwenye safu ya ulinzi kutokana na uzoefu aliokuwa nao,”amesema Aveva.

Kiongozi huyo amesema Mbuyu pamoja na umri mkubwa aliokuwa nao lakini ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na amekuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja hivyo wao wanaamini anayonafasi kwenye kikosi chao ambacho kinapigania ubingwa wa ligi ya Vodacom msimu huu.

Amesema wanamapungufu kwenye nafasi za kiungo mkabaji namba sita na beki wa kulia mchezaji huyo anaweza kuwa mtu sahihi kwasababu anazimudu vyema nafasi hizo na ndiyo maana wanataka kumchukua .

“Kwenye beki wa kulia tunaye Jamvier Bukungu raia wa DR Congo na kati tunaye nahodha Jonas Mkude pekee sasa Twite nafasi zote hizi anazimudu ndiyo maana tunataka kumchukua ili awe msaidizi katika nafasi yoyote kati ya hizo kama kutatokea mmoja wao kuwa majeruhi au kitu kingine,”amesema.

Aveva amesema kwa muda mrefu walikuwa wakimuhitaji mlinzi huyo lakini walishindwa kumchukua kutokana na kuwa na mikataba na klabu yake ya Yanga.

Endapo dili hilo litakamilika itakuwa ni mara ya pili kwa Twite anasajiliwa na Simba, mara ya kwanza alisajiliwa timu hiyo lakini alishindwa kuichezea, licha ya kutambulishwa sikuchache alitua Yanga wakitumia mapungufu machache yaliyokuwepo kweye fomu za usajili uliofanywa na Rais wa wakati huo Ismail Aden Rage.[emoji23]

 
Naona wataka ile huduma yake ya mitupio ya mipira ya kurusha inakuwa kama kona vile
 
Naona una mimba ya Simba sio bure. Kila kukicha Simba hamna timu zingine?
Hili ni Ganda la muwa aveva unakula mswaki waliopigia Wenzio mna nini kwa Twite humo AMA kweli unajiandalia mgogoro
 
Naona wataka ile huduma yake ya mitupio ya mipira ya kurusha inakuwa kama kona vile
Siunajua Mavugo hawezi kufunga mpaka apate mipila ya kurushwa na mtu kama Twite.... [emoji23]
 
Naona una mimba ya Simba sio bure. Kila kukicha Simba hamna timu zingine?
Mwanaume akasiriki haraka kiasi hiko, mithili ya mwanamke mjamzito....

Jibu hoja ya mezani.... Achana na madhambulizi binafsi.
 
Mimi ni Simba lakini uamuzi wa kumchukua Twite siungi mkono. Kwanza ni mkongwe mno umri umeenda! Pili anatokea Yanga hakufukuzwa bado ana mapenzi nayo anaweza kutumika. Tatu aliwahi kuisaliti Simba wakati walipomsajili kwa tamaa za pesa. Kama Simba wanahitaji kiungo mkabaji wapo wengi tena hapa nchini kikubwa ni pesa iwepo na kufanya usajili kwa akili bila mihemko. Ule usajili unaofanywa kukomoana Simba na yanga hauna tija kwa mpira wa kileo. Sajili kutokana na mahitaji ya timu sio kukomoana
 
Huyo Mbuyu labda aje arushe tu mipira ila kwa mfumo wa simba hafai.
 
mnamtafuta mtu wa kumtupia Lawama pindi mkifungwa na Yanga...ameuza yanga yule..
 
Simba na Yanga zikitaka zifike level ya TP Mazembe au Etoir Du Sahel au hata Kaizer Chiefs inatakiwa zipate viongozi wenye Mission na Vision kwenye ishu za mpira, inaonyesha zinaendeshwa kienyeji sana Azam wanakuja vizuri ila waache kuenterntain siasa za usimba na uyanga zinawarudisha nyuma.
 
Hili ni Ganda la muwa aveva unakula mswaki waliopigia Wenzio mna nini kwa Twite humo AMA kweli unajiandalia mgogoro
Wanataka kumuonyesha Rage kuwa mfupa uliomshinda wao wameukamilisha[emoji12]
 
Salum kimenya beki mzuri wa kulia baada ya Juma Abdul
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…