Awamu ya 6 inavyochanga vyema karata kukabiliana na tatizo la ajira nchini kwa kutengeneza ajira milioni 8

Awamu ya 6 inavyochanga vyema karata kukabiliana na tatizo la ajira nchini kwa kutengeneza ajira milioni 8

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
AWAMU YA 6 INAVYOCHANGA VYEMA KARATA KUKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA NCHINI KWA KUTENGENEZA AJIRA MILIONI 8.

Na Bwanku M Bwanku.

Jana Alhamisi Mei 19, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua namna Serikali ya Rais Samia inavyokabiliana na tatizo la ajira nchini. Changamoto ya ajira ni tatizo linalosumbua Dunia nzima kwasasa iwe kwa Mataifa makubwa kwa madogo lakini Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na tatizo hili kwa kuhakikisha inazalisha ajira Milioni 8 zilizoahidiwa kwenye Ilani ya CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu ifakapo 2025 kwa kuendelea kutoa ajira rasmi ikiwemo ajira zaidi ya Elfu 40 inazotoa kwasasa zikiwemo hizi Elfu 32 zinazoendelea kuombwa kwasasa Nchi nzima, huku Serikali ya Awamu ya 6 ikiweka nguvu kubwa pia kwenye Sekta zisizo rasmi (Sekta Binafsi) kwa kuziwekea mazingira mazuri maana ndizo zenye fursa nyingi sana zinazoweza kumaliza tatizo la ajira.

Serikali ya Rais Samia imeendelea kutumia vyema, kimkakati na kimanufaa Diplomasia ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa kupitia ziara za Nje kule Barani Ulaya, Marekani na Falme za Kiarabu n.k kuvuta Uwekezaji wa zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 3.5 unaolihakikishia Taifa ajira zaidi ya Milioni 5 pamoja na Filamu hii ya Royal Tour iliyochezwa na Rais Samia kwenye Vivutio vyetu vya Utalii na maeneo ya Uwekezaji ili kutangaza Uwekezaji wetu na kupata Watalii Milioni 5 ili kukabiliana na tatizo hili la ajira. Pata Nakala yako sasa ya Gazeti letu uone namna Serikali ya Rais Samia inavyoweka Mikakati ya kumaliza tatizo la ajira nchini kwa kutengeneza ajira hizi Milioni 8 na uone jinsi ajira zinavyozidi kumwagwa kila kukicha.

bwanku55@gmail.com
IMG-20220519-WA0040.jpg
 
Mpaka Lipumba anakubali mziki wa Awamu ya 6
 
Back
Top Bottom