Awamu ya Kwanza hadi ya Nne serikali ilitoa fedha za miradi, awamu ya Tano na Sita anatoa Rais - kwanini?

Awamu ya Kwanza hadi ya Nne serikali ilitoa fedha za miradi, awamu ya Tano na Sita anatoa Rais - kwanini?

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
Wadau Nawasalimu.

Naomba kupata Ufafanuzi juu ya Utoaji wa Fedha za Serikali kwenda kwenye Miradi ya Serikali.

Kwanini Siku hizi Hatusikii tena kuwa SERIKALI imetoa Sh.kadhaa kwa ajili ya Mradi fulani badala yake ANATAJWA MTU kuwa katoa hizo Fedha Je hizo Fedha ni Zake Binafsi au za SERIKALI? Je kuna Tatizo gani Kusema SERIKALI IMETOA?

Utaratibu wa Kumtaja Mtu kuwa ndio KATOA kwa Jina ulianza AWAMU ya 5 na sasa unaendelea.

1664451821486.jpg
1664451821412.jpg
 
Serikali nilikuwa instead fedha za miradi na bado inatoa mpaka sasa.

Tatizo,wanasiasa siku hizi wamekosa ushawishi na agenda za kuongea kwa wananchi.

Wanasiasa wanatumia ujio wa fedha ya serikali katika eneo husika kuonyesha kuwa wao au kiongozi fulani ndio kaleta fedha hizo.

Siku wananchi wakielewa kuwa ni wajibu wa Serikali kupeleka huduma kwa wananchi,kuanzia hapo ndio nchi itaanza kusogea kimaendeleo.
 
UPO SAHIHI
ilifika Mahali Wananchi wana Tatizo la barabara Mtu anasema yeye ndio atawajengea
 
Ni kwa sababu hizi awamu mbili zimetawaliwa na unafiki, na uchawa kuliko awamu zote zilizopita. Kiufupi hizo hela ni za walipa kodi! Na siyo za Rais.
 
Hii issue President Mkapa (rip)aliliongelea sana, ni fedha zilizotolewa na serikali na sio na President, kuna mtu alitugeuza watanzania mazuzu, personal sio zuzu
 
Mimi lawama nazipeleka kwa waandishi wa Habari, unaposema Rais unamaanisha ni yeye binafsi. Sijui ndo strategy za kujikomba FIELD YA HABARI IMEOZA WAPO WAANDISHI MIYEYUSHO TU
 
Samia labda anatoa mfukoni mwake. Yaani serikali ipo mfukoni mwake na pesa pia imo humo humo. Ni yeye! Kweli ni yeye! Hata Wabunge anawalipa yeye, ni yeye kwani serikali ipo mfukoni mwake. Akitaka anageuza atakavyo, sasa kuna kosa hapo wakiandika ni yeye!! Majaji pia anawalipa anawateua yeye. Ni yeye kama mfalme.
Kama hamtaki kazuieni kwenye katiba mana ndio inayomuwezesha kufanya hivyo. Ni yeye mana akikataa haitoki Ng'o... Nani anabisha kuwa ni YEYE.
Kazi ipo, harafu watu wanapinga mabadiliko ya kagiba!
Kumbuks na tambua katiba ndio inaweka serikali mfukoni mwa rais (sasa utajaza mwenyewe mfuko wa rais-sa100 upo wapi). Hata Nyerere enzi zake alichukia sana kusikia mzungu mmoja akisema eti serikali ipo mfukoni mwa mzungu huyo!! Alimuonyesha cha moto, alimpa masaa24 awe amtoka nchini, mana Nyerere alitambua serikali ilikabidhia mfukoni mwake sio mfukoni kwa mzungu. Kuna mipopoma hapa haitanielewa!!
 
Wadau Nawasalimu.

Naomba kupata Ufafanuzi juu ya Utoaji wa Fedha za Serikali kwenda kwenye Miradi ya Serikali.

Kwanini Siku hizi Hatusikii tena kuwa SERIKALI imetoa Sh.kadhaa kwa ajili ya Mradi fulani badala yake ANATAJWA MTU kuwa katoa hizo Fedha Je hizo Fedha ni Zake Binafsi au za SERIKALI? Je kuna Tatizo gani Kusema SERIKALI IMETOA?

Utaratibu wa Kumtaja Mtu kuwa ndio KATOA kwa Jina ulianza AWAMU ya 5 na sasa unaendelea.

View attachment 2371573View attachment 2371574

Haya ni madhara ya siasa za kijinga, na ulevi wa madaraka wa siasa za Magufuli. Kwa sasa huyu mwingine anaiga tu akiamini ndio atakubalika. Yaani CCM walitengeneza propaganda kisha wakaiamini wenyewe.
 
Mimi lawama nazipeleka kwa waandishi wa Habari, unaposema Rais unamaanisha ni yeye binafsi. Sijui ndo strategy za kujikomba FIELD YA HABARI IMEOZA WAPO WAANDISHI MIYEYUSHO TU
Kama msemaji wa serikali katamka hivyo bila ufafanuz, mwandishi wa habari hana jinsi ya kuhoji akihofia kushughulikiwa. Hapa ndipo unaona mipaka ya siasa katika kushughulikia wananchi. Kinachotokea ni siasa zile za kampeni ambazo zilitakiwa zisitishwe siku moja kabla ya kupiga kula, lakini zimeachwa kuendelea mpaka raund ingine ije. Mie naita ni URAFI WA MADARAKA.
 
Hii ni kutokana na baadhi ya watanzania journalist na viongozi wetu ni wanafiki mazuzu na wenye njaa Kali
Na hii tabia inaondoa uzalendo uwajibikaji na team work katika taifa
Bad enough baadhi ya mihimili mingine inajipendekeza kwa rais
Rais inabidi awe wa Kwanza kukemea hili ,Kama anataka kujenga taifa lenye uzalendo na lenye kujitambua
Uzalendo sio kujipendekeza kwa rais au serikali Bali ni kuipenda nchi na taifa lako kuliko kitu chochote
Rais na serikali ipo kwa muda
Mfano,Rais Nyerere na serikali yake na Marais wengine wako wapi ?
Lakini nchi na taifa la Tanzania lipo na litaendelea kuwepo
Hii tabia ilionzishwa kwenye awamu ya tano ni ya kinafikii na ya kipumbuvu
Inabidi ikemewe na kukataliwa kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom