Awamu ya kwanza udahili vyuoni inafungwa Agosti 5, 2021; vijana bado wapo makambini JKT

Awamu ya kwanza udahili vyuoni inafungwa Agosti 5, 2021; vijana bado wapo makambini JKT

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
7,602
Reaction score
7,332
Round ya kwanza ya udahili inafungwa August 5, 2021 hadi leo vijana walioitwa JKT kwa mujibu wa sheria wamefungiwa makambini (mf. Mgambo).

Inabidi wengi wajaziwe na ndugu au rafiki zao. Hawana muda wa kujua kwa umakini ni nini kile wanataka na wengine hawapati ushauri wa kutosha. Hii ni hatua muhimu katika maisha ya binadamu.

Hivi JKT wanashindwaje kuwapa siku za kutosha wakakamilishe hili zoezi. Na TCU/ NACTE wako wapi kwenye hili. Tukumbuke matokeo hutolewa vijana wakiwa kambini na mategemeo ya wengi huwa tofauti na hali halisi.

Je, una ushuhuda wowote kuhusu hili?
 
Mgambo walikuwa wana wapa ruhusa kwenda kuomba vyuo on individual application basis. Kama hukuomba hakukuwa na ruhusa ya jumla . It is too late now to effect that. Pole.

Kuna round ya pili, utilise that please, nenda Mgambo andika barua ya kuomb kijana uende anye afanye hiyo task watakukubalia. hata vijana wenyewe walikuwa wanaomba wanaruhusiwa.
 
Nimekuelewa mkuu lakini nilifikiri policy ingekuwa kuwapawote ruksa.
 
Mimi nafikiri huko makambini wangekuwa wanarndesha semina kwa hawa vijana juu ya vipaumbele cha taifa na fani zenye fursa kubwa.

Ikiwezekana watambue ufaulu wa kila kijana na umahiri wa kila kijana then wawape mwanga wa kipi wafanye na kipi wasome. Ni kazi kubwa ila si ndio kazi ya malezi kwa vijana tegemeo la taifa, waifanye tu.

Inasikitisha kijana amekaa JKT miezi mitatu hajui hata uelekeo uwe upi kimaisha, sasa atakuja vipi kujitegemea na kutegemewa?.
 
Back
Top Bottom