Awamu ya pili ya ufukuaji wa maiti yaanza Shakahola

Awamu ya pili ya ufukuaji wa maiti yaanza Shakahola

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amewasili katika kaunti ya Kilifi kuongoza awamu ya pili ya ufukuaji wa maiti katika shamba la Shakahola. Shughuli hiyo iliyokuwa imesitishwa kwa muda kutokana na mvua kubwa zinazoshudiwa kaunti humo, inaendeshwa na kikosi maalum cha idara ya upelelezi wa jinai DCI.

Mpaka kufikia sasa Jumla ya miili 112 imefukuliwa huku uchunguzi wa awali wa maiti ukionesha kuwa wengi walifariki dunia kwa kunyongwa.

Haya yanajiri huku moja kati ya washukiwa wakuu wa Mchungaji Ezekiel Odero akitarajiwa kuwasilishwa ombi katika Mahakama ya Mombasa, alitaka wamuzi wa awali wa kumfungia akaunti zake za Benki kubatilishwa.

20230509_124023.jpg
20230509_124016.jpg
20230509_124019.jpg
20230509_124021.jpg
20230509_124738.jpg
 
Jamaa alikua anaua halafu wanasema ni utashi wa watu kufunga hadi kufa.

Jamaa mjanja sana.
 
umbwa kabisa hiyo pasta inatakiwa na yenyewe waiue ili ikaonane na jesus ,
 
Nilijisemea huenda kawauwa na kuchukua mali zao
Kumbe kweli
Ukiangalia crime cases utajua kabla hata kesi hawaja solve
 
Maiti zingine hazina viungo vya ndani.
Inaonekana mtandao ni mkubwa Sana jamaa alikuwa anavuna viungo
 
Ila watu wakenya wanavisa sana yaan mambo yao huwa ni makubwa makubwa saaana ukitazama citizen tv ndo utajia akili zao zinawatosha wenyewe.
 
Back
Top Bottom