Awamu ya Sita ni awamu ya Katiba

Awamu ya Sita ni awamu ya Katiba

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kama kuna kipindi ambacho Katiba yetu imelivusha taifa letu basi ni kipindi hiki cha kuwapata viongozi wetu wakuu wa awamu ya sita. Katiba yetu hii imepata heshima kubwa duniani kote na kuifanya Tanzania iheshimike sana Afrika na duniani kote. Tuwatambue hadharani na kuwapa heshima viongozi wetu walioiheshimu Katiba hadi tukapata viongozi wapya bila misukosuko wala kuyumba baada ya kuondokewa ghafla na Rais wetu JPM; Imetuonyesha kuwa taifa letu limekomaa, wametutoa kimasomaso. Lakini ni vizuri pia tuwatambue hadharani na kuwapa adhabu bila kusita watu wote wanaovunja Katiba yetu hii iliyotutendea jambo kubwa hivi.

Kipindi hiki kimetuonyesha sote umuhimu wa kuwa Katiba safi, iliyonyooka na inayokubalika na wote. Hivyo, kila mtu atashangaa kupitiliza kama Rais Samia na Makamu wake Dkt Mpango hawatamalizia ubororeshaji wa katiba yetu hii ambayo ndiyo iliyowafikisha hapo walipo sasa. Katiba bora italinda muungano, kukuza demokrasia na kulinda mafanikio yaliyopo na yajayo.

Tunategemea viongozi hawa wa kikatiba watupatie Katiba safi mpya ndani ya siku zao 100 za kwanza, na hatutegemei wao wawe wa kwanza kuvunja katiba.
 
Back
Top Bottom