Awamu ya Sita ni ushahidi safi wa utii wa Katiba yetu tunayoapa kuilinda

Awamu ya Sita ni ushahidi safi wa utii wa Katiba yetu tunayoapa kuilinda

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Awanu ya sita ni awamu ya Katiba, ni ushahidi tosha kuwa kutii na kuheshimu Katiba ya nchi kunalipa sana. Taifa limevuka salama baada ya kifo cha Mh. Rais Magufuli kwakuwa Katiba yetu haikupepesa macho juu ya Rais ajae baada ya Rais aliyeko kubata bahati mbaya. Katiba yetu ndiyo Nyangumi wetu aliyetuvusha kutoka kwenye maji marefu yaliyojaa papa wengi kwenda nchi kavu.

Hivyo ni wito wangu kwa viongozi wote wa Awamu ya Sita kuwa waendelee kuiheshimu Katiba kwa 100% kuliko awamu zote zilizopita. Viongozi wa awamu ya 6 waitekeleze Katiba mstari kwa mstari, kifungu kwa kifungu na ukurasa kwa ukurasa, na ikiwezekana waiboresha sana kuliko ilivyo sasa ili kuondoa maeneo yote kwenye Katiba yasiyotutakia mema kama taifa.

Itakuwa sio sawa kama Katiba tunayoapa kuilinda inaruhusu uhuru wa vyama vya siasa, uhuru wa habari, uhuru wa kujumuika, uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa, uhuru wa kupiga kura na kupigiwa kura, na uhuru wa kuishi lakini kuna kiongozi au mtendaji kwa utashi wake na sababu zake anaamua kuzuia na kuuminya uhuru huo. Kufanya hivyo ni kukosea sana, maana inaonekana unachagua kuheshimu zile sehemu tamu kwako za Katiba na kuchukia sehemu chungu kwako za katiba.

Awamu hii ya 6 lazima ifanye mengi sana kuhusu Katiba yetu hii.
 
Wale majambazi wanaojiita wabunge wa Chadema kule bungeni wanatia doa hilo bandiko lako

Sent using Jamii Forums mobile app
kama katiba inasema mbunge lazzima awe mwanachama fulani hakuna namna lazima awe mwanachama, ukimfumbia macho umevunja katiba. Lakini kitendo cha kufurahia ibara inayokuingiza madarakani na kuchukia ibara inayoruhusu uhuru wa vyama vya siasa kufanya siasa sio sawa hata kidogo. Katiba ni "all or none" kula muwa wote au acha muwa wote, usiache sehemu zile nguvu za muwa na kuzipa jina la hovyo la "vifundo"

Kiongozi safi anapimwa kwa kutekeleza mistari, ibara na kurasa zote za Katiba iliyomuingiza na aliyoapa kuilinda.
 
Back
Top Bottom