Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Tunasema tunataka kukuza ajira kwa vijana, tumepata mikopo kwa ajili ya kukuza Teknolojia. Tunasema Teknolojia ndio kila kitu kwa Dunia ya sasa, tunashauri vijana wajifunze na kuwekeza kwenye teknolojia, ni Vema na Haki, yet tunasababisha kitendea kazi muhimu (bundle) kisishikike; hapo tunajenga au tunabomoa.
Internet Bundles
Dunia ya sasa ni (Information at your fingertips), kila information unaweza ukaipata bure mtandaoni. Unaweza ukajifundisha mwenyewe jambo ambalo lingewachukua watu wa karne za nyuma miaka kulifanyia research leo unaweza ukalifanya kwa siku. Ni kama kipindi kile cha Maktaba kila mkoa ili watu wajifunze hii ndio maktaba ya leo. Kama kipindi kile ambapo hatukugeuza Maktaba kama kitega uchumi cha kuongeza pesa ni vema tusigeuze hii Source of Information kama kibubu cha kujichotea Pesa.
Je, Gharama za Bundle ni Kosa la Serikali au Mitandao, nani wa kulaumiwa?
Unaweza kusema watu wa mitandao ni wezi, si kweli, sababu ni Serikali ndio imeamua kutoa bei elekezi kwahiyo hizo bei ni maelekezo ya Serikali, na unapotoa bei elekezi ushindani unapatikana vipi? Kulikuwa na kipindi cha offer za Vifurushi vya Bundle za Bure mida fulani au hata usiku, sasa ukipangia watu bei elekezi na kila mshindani akafuata hizo bei unadhani kuna umuhimu wa mtoa huduma kutoa offer / vifurushi?
Kipi Kifanyike
Ni rahisi sana;

- Serikali ina kampuni yake TTCL na nyingine ambayo wana share nyingi Airtel, kwanini wasiwekeze huko na kufanya shamba darasa na kushusha bei kama wanavyotaka ili iwe mfano?
- Pili, Serikali iwaache hao wengine wajivinjari kama wanavyojua bila kuwapangia wala kuwaingilia, ili nguvu ya soko ipange bei hata wakifanya cartel Serikali ina TTCL itabakia bei za chini watu watahamia TTCL.
- Kwa kutumia kampuni yao hawashindwi kuweka free surfing kwa mitandao kama Youtube kwa ajili ya watu kujifunza hata masaa ya usiku au zile freeware softwares kuzifanya mtu aweze kuzi-download bure.