Awamu ya Tano: Wakandarasi wamedharaulika sana

Awamu ya Tano: Wakandarasi wamedharaulika sana

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
20191215_225052.jpg
Katika utawala wa Awamu ya Tano, kwa makandarasi mambo ni magumu sana.

Ukandarasi maana yake ni kufanya kazi kwa ajili ya mtu mwingine (sasa ni serikali), kimkataba.

Makandarasi ni kada iliyoenea nchi nzima, na kada hii imetumika sana katika kampeni Awamu ya Nne ili kuiingiza Awamu ya Tano madarakani.

Sasa hivi siyo siri makandarasi wanadhalilika na kudharauliwa.

Umoja wa makandarasi ulitoa masikitiko hivi karibuni juu ya mtizamo hasi unaoonyeshwa na viongozi wa Awamu ya Tano lakini muda mfupi baadaye tukaona ya Jaffo.

Waswahili walisema tenda wema usingojee shukrani na kwa makandarasi wajijue kuwa akili ni mukichwani mwao.
 
Awamu ya tano ndio wakandarasi wamepiga hela kuliko awamu zote...

Magufuli anaijali sana sekta ya ujenzi, pesa nyingi sana zinapelekwa huko.

Sema kama hao hela wameshirikiana kula wengi kule halmashauri ila msala unamkuta yeye binafsi..

Akiomba milioni miambili halmashauri anapewa million 100 ila anasaini miambili hiyo mia nyingine kuna watu wanakula ukigoma hupewi hela.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule alijenga banda la kuku kwa mil 100 alikuwa ana mdharau nani !?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ujinga uliokithiri kwa watanzania kama posti hii kufikiri miradi inasimamiwa na mawaziri.

Jiulize aliyetoa tenda alikuwa wapi, msimamizi alikuwa wapi, na mkandarasi kwani alienda kuvunja benki kulipwa hizo shs 100milioni?

Udhaifu wa serikali kushindwa kusimamia miradi yake sasa ni dhahiri.

Inabidi mawaziri waache kazi zao waende site ili wagundue kuwa walioajiriwa kufanya kazi ya usimamizi wa miradi kimkataba wanalipwa bure.
 
Wewe utakuwa na matatizo makubwa kwenye akili zako!
Anachojaribu kukueleza ni kwamba, inawezekana vp mkandarasi alipwe milioni 100 ilihali analipwa baada ya kuissue certificate? Sasa upande wa serikali ulikuwa wapi hadi mtu anaissue certificate ya m100 kwa kazi ya m4? Ww unaona ni sawa?
 
Awamu hii wakandarasi wameula Sana , huwez kuta civil engineering yyte anaranda mtaani kazi kibao , Sisi wa kajamba Nani ndo tunasota , changamoto ni kuwa karbu nusu ya bajeti inaelekezwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu na Kwa vyovyote vile lazima iwe monitored Sana , na mkandarasi ndo victim wa Kwanza endapo mambo yakienda mrama
 
Back
Top Bottom