We sijui hua akili yako kama iko na logic kweli....
unakuja hapa kunipatia sababu za kijinga kama high fuel cost, kwani ET na wengineo hawanunui mafuta? Kampuni kama American airlines, Southern airline,Delta hunua refurbished planes Kwa bei ya Chini na kuzitumia kaa mchezo....
ATCL haina hata ripoti moja ya performance na unataka Ku inside Kwa discussion, haina hata safari moja ya nje ya bara, bado haijapewa leseni na IATA,
Kwa upande mwengine Ethiopia ndege hununuliwa na serekali, hatujui true fleet ownership ya ndege za ET manake kama Tz, Ethiopia haichapishi data yoyote kuhusu Kampuni hio.... ET pia hawalipi body yoyote ya serekali kutumia Bole airport ..
Wakati huo huo, KQ inalipa zaidi ya $400m kutumia JKIA, mbali na hapo, spare parts hulipishwa Kodi wanapoagizia kutoka nje.
Fleet ownership ya least planes inagharimu KQ $140m kila mwaka for 20 planes!!!!!
Tukichua average plane cost ya kununua ndege moja ya KQ at $170m (it's probably higher than that)
Alafu tupige hesabu ya Ku lease those 20 planes for 25 years VS buying those planes and running them for 20 years which is about the AVG life span of those commercial planes
Leasing = $140m * 20 years = $2.8B
Buying = $170m * 20 planes = $3.4B
Hebu niambie, Kwa Kampuni ambayo ni publicly listed Kwa stock exchange , ambayo inafaa kununua ndege zake na pesa zake na kuzilipua na revenue, which is better? Kulipia hela ndogo ndogo kila mwaka au kununua ndege za thamani ya $3.4B Kwa mpigo!!!! Mwanzo hizo hela watazitoa wapi? Na hata kukitikea malaika na waweze kuchangisha hizo hela, Kampuni itakua haina liquidity watakua hawajabakisha hela yoyote ya kulipa wafanyikazi wala kununua mafuta, watakua wana ndege lakini kuzipeperusha hawana uwezo .....
Alafu pia usisahau thamani ya ndege pindi unapoinunua inaanza kushuka , hata Ile drimliner yenu tangu mwaka Jana Hadi sasa mkingojea safari ya ndia na China, thamani ya hio ndege ishashuka, itafika mahali iwe imechoka hapo mkitaka kugeuza na mchukue ndege mpya ndo mtapiga hesabu na muone haziingiliani, utakuta ndege mliinunua Kwa $250m pesa za walipa Kodi lakini haijaleta faida ya $250m + kulipia mishahara ya wafanyikazi ndani ya hio ndege + gharama ya mafuta yaliotumika kusafiri ..
Tofauti na leasing kama ile KQ wamechukua ya maximum of 25 years, ikifika hapo ndege inaregeshwa Kwa Kampuni husika. Tena isitoshe ukiona ndege haifurahishi unaweza kuiregesha Kwa hio Kampuni na uchukue nyengine mpya na uendelee kuilipia ....
Kwasasa vile KQ imetoka Kwa shida ya loss kubwa kubwa, inapanga 100% fleet expansion by 2024 ili Ku compete na ET, Yani ndege ishirini zitaagiziwa ili kupata discount, Hebu niambie kama unaweza agizia ndege 20 na uzilipie cash!!! Hata kama ni pesa za walipa Kodi, JPM hawezi thubutu kutoa zaidi ya $3B kununua ndege ishirini Kwa cash!!!