siyo kila unachokitaka utakipata kwa 100%hapo zamani za kale kulifanyika uchaguzi wa kiongozi watu!
kiongozi huyo alitakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
-awashinde wote kwa mali,
-awashinde wote kwa akili,
-awashinde wote kwa urefu,
-awashinde wote unene,
-awashinde wote kwa watoto
lakini uchaguzi wao ulishindikana, maana hawakumpata mtu wa sifa zote hizo!
hadithi hii inapatikana katika kitabu cha darasa la pili cha zamani zetu!
lakini nikiangalia kwa undani, kuna funzo kubwa sana hapo, ambalo hadi sasa bado lipo na lina'hold!
unadhani huyu mtunzi wa miaka hiyo wa kisa hicho anatufundisha nini kwa tanzania ya leo, na hali halisi ya chaguzi zetu za viongozi wa sasa?
Sijakuelewa kabisa ndugu yangu!!Huyu mtunzi kachangia kiasi kikubwa kudumaza akili za wa tanzania, watoto kabla ya kufikia darasa la pili walijiamini wanweza kuwa na sifa zote ulizotaja;
Watoto ukiwa encourage watajiamini kuwa na uwo uwezo wa uliotaja;
Akili
Uwezo
Urefu(kama anaotayari)
Unene (afya)
Watoto wengi ( sensiof belonging)
Vitabu kama hivi inabidi vichomwe mote havisaidii katika jamii zaidi ya "Can't do attitude" ambazo watz wengu tunazo, vinalengo la kukuza generation isiyo jiamini.
Tunaweza kuwa na kuwapata viongozi wenye sifa zote za kutuongoza hapa tanzania kama tutakiweka pembeni katabu hicho, kwani wapo wenye sifa zinazo takiwa.
Sijakuelewa kabisa ndugu yangu!!
Hadithi ile inasema, hakuna mtu mwenye sifa zote zile...kwakuwa nyingine ni za kijinga na ndio maana hawakuweza kumpata. Wewe unasema kitabu kile kilipaswa kichomwe moto? Labda nimechoka na mihangaiko ya leo.... sijakuelewa Monsieur
Sijakuelewa kabisa ndugu yangu!!
Hadithi ile inasema, hakuna mtu mwenye sifa zote zile...kwakuwa nyingine ni za kijinga na ndio maana hawakuweza kumpata. Wewe unasema kitabu kile kilipaswa kichomwe moto? Labda nimechoka na mihangaiko ya leo.... sijakuelewa Monsieur