Aweso awaasa DUWASA, Msizoee shida za wananchi

Aweso awaasa DUWASA, Msizoee shida za wananchi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amewaasa wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuacha kuzoea shida za wananchi, na badala yake kuzitafutia ufumbuzi ili wananchi wapate huduma ya Majisafi ya uhakika.

Waziri Aweso amewaasa wafanyakazi hao wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu Baraza la Saba la Wafanyakazi wa DUWASA lililofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Tume ya Maadili, ambalo pamoja na mambo mengine limepitia Rasimu ya Bajeti ya Mamlaka hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Aidha Aweso amesema wananchi watapata huduma bora iwapo wafanyakazi na Menejimenti watafanya kazi na kutekeleza wajibu wao kwa ushirikiano, kusikilizana, na kuepuka upendeleo ambao huzaa manung'uniko mahali pa kazi na kushusha ufanisi. Asisitiza Aweso,"Muwe na utamaduni wa kuneneana mema".
 
Back
Top Bottom