AY amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Remy aliyeishi nae kwa miaka nane

Hongera AY kwa kutuchukulia dada yetu naamini umepata jiko zuri

Sent from my GT-N7000 using JamiiForums mobile app
 
Miaka nane uchumba huo au sjui ni nini ?
 
Mhuu,.ana moyo mwe 8yrs c umesoma mpaka PhD!??...Anyways hongera kwao ni jambo jema sana wabarikiwe.
 
Sasa kama amesha ishi naye miaka 8 pete ya uchumba ya nini,hapo kinachotakiwa ni kuoa tu hiyo stage ya pete ya uchumba wameshaivuka tayari,au mie ndio sielewi...
Unaelewa na unajiuliza kwa haki.
Hivi huu uzungu unaingiaje kwenye tamaduni za kiAfrika?
Mchumba utaishi naye na kuzaa?
Ama mwanamke unayeishi naye kama mke, unawezaje kumvisha pete ya uchumba?
Maadili tunayaporomosha makusudi tunapoyapaka mafuta baadhi ya mambo ya hovyo yanayoenda kinyume na tamaduni zetu.
Neno linalomstahili kwa tendo hilo alilolifanya huyo mbongo fleva ni kuwa...."Anataka kubariki ndoa na kimada wake aliyeishi naye zaidi ya miaka 8".... Lakini hii ya kusema kamvisha pete mchumba wake waliyeishi naye zaidi ya miaka 8 ni matusi ya nguoni na ni kufuru kubwa sana ya mmomonyoko wa maadili inayobungua utamaduni wa kiAfrika.
 
Chama la wana lidumuuu
SHAKE BEFORE USE
Kama prof K 13yrs
AY 8 yrs
[emoji23]
 
mpaka wamefanana Khaaa miaka 8.... mimi booking mwisho miaka mi3 kama huna sababu za msingi jikatae..
chaaa

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
Hiyo miaka 3 grace period?? Naomba niwekeze hapo aisei..
 
Hebu ngoja tuanzie hapa Nina wasiwasi na hiyo miaka 8 ,alikuwa na demu mkenya Anaitwa Amani baada ya kumpiga chini akawa na flaviana Matata baada ya hapo ndio tukaanza kusikia Habari za Mnyarwanda
 
Huyu kijana nilikuwa namuona anajitambua kumbe nae ni popoma mduanzi.
Unakaaje na binti wa watu kwa miaka Nane (8) bila kufunga nae pingu za maisha!?
Halafu unawahadaa wazazi wake kwa kumvisha pete ya uchumba baada ya miaka yote hiyo! Akitokea mjanja wa mjini akataka kuoa kabisa amuhamishie Dubei utakwazika!? Maana huyo binti bado ni asali,tena ya nyuki wadogo.
Shubaaaamit AY.
 
Baada ya kuona wakina dada mmezidi dramas, sasa ni mwendo wa 5 years plus katika mahusiano ya urafiki, then baada ya hapo ndo suala la uchumba linawekwa mezani. Hii kampeni inapaswa kuendeshwa nchini pote, itapunguza hali za kushtukiza za hawa wenzutu pindi tukiwa katika mahusiano. Miaka mitano mtu unakuwa atleast umemjua in and out for almost 60%
 
Uzungu mwingi sana siku hizi

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
AY miaka 8
Prof J miaka 13
Diamond Miaka 20

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…