AY na Mwana FA waingia kortini

jipu sugu

Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
8
Reaction score
4
Kuna uwezekano mkubwa, AY na Mwana FA wamefungua kesi ya masuala ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi zao.



Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amepost picha Instagram akiwa kwenye mahakamu kuu ya Tanzania akiwa na rappers hao. “At the High Court of Tanzania, Dar Es Salaam. #UsijeMjini #DakikaMoja #Tigo #CopyrightsInfringement #stoppingwizi @aytanzania @mwanafa,” ameandika Msando.

Kuna uwezekano kuwa nyimbo zao Usije Mjini na Dakika Moja zikawa zimetumiwa na kampuni bila ridhaa yao. Makosa ya kukiuka haki miliki kwenye kazi za sanaa huadhibiwa zaidi kwa kwa faini.

Chanzo: Bongo 5
 
ahahahh wanasubiri kukinga bakuli mamilioni ya mwagike kiulainiii baada ya kushinda kesi

watoe nyimbo mpya na kali wauze.

japo kama wameibiwa kazi zao wanahaki ya kushitaki
 
si mpaka washinde mkuu unadhani kampuni kama tigo nao watakubali kirahisi
 
Hiyo ni sawa kama kweli wameona haki zao zimepokwa,na watachukua mpunga mrefu sana. Lakini wajiandae kwa upande wao kama kibao kikiwageukia itawabidi wao ndio walipe gharama za uendeshaji wa kesi.
 
SIJUI WAMEJIPANGAJE NA PRODUCER WA HIZO NYIMBO..MAANA WANAWEZA KUINGIA KORTINI UKAKUTA BEAT ALIUZA PRODUCER KWA WATU WA HIYO KAMPUNI NA WAO KAMA WASANII HAWANA HAKIMILIKI YOYOTE KWENYE MAPIGO YA VYOMBO...REFER WIMBO WA FREEDOM WA MR. BAYSER NA SUGU...BEAT NA CHORUS NI MALI YA PRODUCER MARKO CHALI CHINI YA MJ RECORDS ...HATA MIE NAJIPANGA NIKAINGIZE VOCAL KWENYE FREEDOM..ITAITWA DIRTY VERSION....FEATURING NEY WA NITEGO NA MSAGA SUMU.
 
FA ANANIANGUSHA BANA...MAVAZI GANI HAYO ANATINGA NAYO HIGH COURT?....HUKO KWENYE BIASHARA UNATAKIWA UNAPIGA BIZNESS SUIT KALI....HATA UNAOWADAI WAKIKUONA WANAJUA KWELI LEO LAZIMA SADAKA ITOLEWE MAANA WADAI WAPO KI-BIASHARA ZAIDI.
DOGO NEXT TIME USIRUDIE KOSA HILO...VAA DRESS CODE INAYOMAANISHA UNACHOKIONGEA AU UNACHOKITARAJIA.
 
Msando Mmenye angalia usiwaingize choo cha kike Masawe na kimario.
 
Hii itaweka Precedent kwa wanamuziki wengine namna ya wao pia kwenda kudai haki zao.
 
Hii ishu haiishi tu.
Nadhani ilitokea mwaka juzi kwa Tigo kutumia wimbo wa bila ridhaa yao.
 
si mpaka washinde mkuu unadhani kampuni kama tigo nao watakubali kirahisi
Tatizo sio kua tigo ndio watakubali inatakiwa mahakama ndio itoe uamuzi as long as wameshalifikisha swala lao mahakamani basi maamuzi ya mahakama ndio yatakayoamua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…