Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha, ametolea ufafanuzi madai ya baadhi ya watu wanaoishutumu TBC kwa kutovialika baadhi ya vyama vya upinzani, ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kushiriki mijadala inayohusu siasa.
Akijibu shutuma hizo, Dkt. Rioba amesema kuwa katika kipindi cha Mizani, ambacho hujadili masuala mbalimbali, ikiwemo siasa, aliwahi kufanya juhudi za kuwaalika viongozi wa CHADEMA kushiriki, lakini juhudi hizo zilishindikana. Hata hivyo, baadaye alifanikiwa kufanya kipindi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Benson Kigaila.
Aidha, ameongeza kuwa vyama vyote vya upinzani nchini vinafahamu kuwa TBC ni chombo chao cha habari na vinakaribishwa muda wote.