Sijasema ligi imekwisha ila kwa jinsi walivyojipanga nakuhakikishia mkuu hiyo timu (Azam) itachukua ubingwa. Na pia timu hii itapiga hatua kubwa kimaendeleo na kuziacha simba na Yanga mbali sana.Najua kuna baadhi ya watu wanaumia kutokana na kauli hii lakini huo ndio ukweli. Timu zina miaka sabini lakini bado ombaomba? Una rasimali watu ya wapenzi, mashabiki na wanachama zaidi ya milio tano halafu unakuwa ombaomba? Aliewaroga Simba na Yanga nafikiri amekufa, angekuwa hai angewasamehe bure. Kwa Yanga wanateseka na laana ya marehemu Tabu Mangara.Huyu mtu alileta maendeleo makubwa ndani ya yanga.Ndie aliefanikisha ujenzi wa lile ghorofa pale jangwani na kununua magari manne kwa ajili ya timu. Fadhila aliyopata ni kufukuzwa kwa bakora. Alipofukuzwa muda si mrefu Yanga akapigwa 6-0 na simba. Kwa upande wa simba bado naifuatilia historia yake.ushauri wa bure kwa yanga waende kutambika kwenye kaburi la Tabu Mangara.