Azam & DStv punguzeni kidogo vifurushi vyenu kipindi hiki Cha CORONA.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wateja wenu wanapitia hali nguvu kiafya na kiuchumi, hebu punguzeni kidogo bei za vifurushi Kama sehemu ya kuungana na wateja wenu kwenye hili.

Hii ni pamoja na makampuni ya simu za mikononi kwakuwa wateja wenu inawabiti kufanyakazi wakiwa majumbani kupitia simu au Internet.

Msijifanye Kama vile hamuoni hali za wateja wetu katika kipindi hiki. Rafiki wa kweli ni wakati wa dhiki. Rudisheni kidogo kwa wateja wetu ili urafiki uwe wa kweli.

Hakika nitahamia kwenye mtandao na tv itakayoshusha kidogo vifurushi vyake
 
Na wale dada zetu jaribuni kupunguza gharama na wale wenye gesti hebu kaeni muelewane ili walau wateja wenu tumudu gharama
 
Wateja wenu wanapitia hali nguvu kiafya na kiuchumi, hebu punguzeni kidogo bei za vifurushi Kama sehemu ya kuungana na wateja wenu kwenye hili.

Hii ni pamoja na makampuni ya simu za mikononi kwakuwa wateja wenu inawabiti kufanyakazi wakiwa majumbani kupitia simu au Internet.

Msijifanye Kama vile hamuoni hali za wateja wetu katika kipindi hiki. Rafiki wa kweli ni wakati wa dhiki. Rudisheni kidogo kwa wateja wetu ili urafiki uwe wa kweli.

Hakika nitahamia kwenye mtandao na tv itakayoshusha kidogo vifurushi vyake
Hii thread ina AKILI SANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wao wanapitia kipindi kigumu maana athari zinagusa kila idara...kama wateja hawana uwezo wa kulipia kifurushi Basi na wao hawawezi kuendesha kampuni wala kuwalipa wafanyakazi.

Sehemu sahihi ya kulilia shida zako kwa sasa ni Serekalini tu, kama inabajeti ya kukabiliana corona Basi iwape wananchi ruzuku kwenye huduma mbalimbali za kijamii..mfano umeme,maji, afya na mengineyo.

Kuwalilia Azam ama Dstv sawa na kumlilia Mangi kwenye kibanda chake kuwa apunguze bei ya sukari kwa sababu wewe mteja wake wa kila siku..
 
Hiyo mifano yako haifanani, makampuni haya yameshalimbikiza faida kubwa kipindi kile Cha amani, hivyo hayawezi let say kutoza vifurushi vyao kwa nusu au robo tatu ya bei ya kawaida kwa kipindi Cha siku 30 au 60 za amri ya kubaki nyumbani kuepusha COVID-19. Hii itakuwa na faidi mbili kwao 1. Kuwezesha wateja wao wamudu kuendelea kulipia vifurushi wakati uchumi wao umeyumba. 2. Itakuwa sehemu ya customer care na kuwabakisha wateja wao hata wakati wa hali ngumu. 3. Watapata sababu/justification ya wao nao pia kuomba ahueni ya tozo toka TRA na mamlaka nyingine katika kipindi hiki.

Hii kaka ni tofauti na kiduka Cha mangi pale mtaani.
 
Dstv wameshusha mbona. Chaneli zilizokuwa zibapatikana kwenye vifurushi vikubwa zimewekwa pia kwenye vifurushi vya bei ndogo.
 
DStv nadhani wameshusha kidogo maana nilishusha kifurushi mpaka bomba ila nashangaa bado napata SS3 na 4
 
Back
Top Bottom