Klabu ya Azam FC imetwaa Kombe la Shirikisho la
Azam Sports Federation Cup, baada ya kuichapa Lipuli FC bao 1- 0 katika mchezo wa Fainali ulifanyika leo Juni 1, 2019 kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.
Iliwachukua Azam FC, hadi dakika 65' kipindi cha pili kupata bao lililowekwa kimiani na Obrey Chirwa.
Azam FC, imeweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa Kombe la
Azam Sports Federation Cup kwa mara ya kwanza kihistoria ya klabu hiyo, hivyo kukata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Kimataifa kwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, (CAF CONFEDERATION CUP) msimu wa 2019/2020.
View attachment 1114294