Azam FC v Kagera Sugar na Toto Africans v African Sports

Makoye Matale

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
6,491
Reaction score
2,104
Baada ya jana kushuhudia mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga kwa mara nyingine tena wakiwapitisha kwenye shamba lenye mbigiri wagonga nyundo Mbeya City FC, ligi hiyo inaendelea tena leo katika viwanja viwili. Azam FC watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kutoka Bukoba a.k.a 'Katerero City' huku Wanakisha Mapanda Toto Africans ya Mwanza wakiwakaribisha watani na ndugu zao wa damu African Sports kutoka Jijini Tanga.

Source: https://twitter.com/Tanfootball/status/681031711229120512

Michezo yote itaanza saa 10 jioni, tukutane hapa tutupie Live Updates.
 
Mechi imeshaanza na sasa ni dakika 2 Azam 0-0 Kagera Sugar.
 
Kule Mwanza ni dakika ya 2 Toto Africans 0-0 African Sports.
 
Dakika 9: Tche Tche anaandika bao la 1; Azam 1-0 Kagera Sugar.
 
Dakika 20: Azam 1-0 Kagera Sugar
Dakika 18: Toto 0-0 African Sports
 
thanx for updates

Karibu sana Mkuu. Nimeshindwa kuendelea kuleta updates baada ya TANESCO kufanya mambo yao. Wakuu wengineo mnaoshuhudia mechi hizo endeleeni kutupia updates.
 
Hadi HT:

Azam 1-0 Kagera Sugar
Toto Africans 0-0 African Sports
 
HT:Ashanti United 0 - 0 Kiluvia United.Ligi daraja la kwanza ,uwanja wa Karume Dar.
 
Dak. 52: Azam 1-0 Kagera Sugar
Dak. 51: Toto 0-0 African Spirts
 
Dak. 65: Azam 1-0 Kagera Sugar
Dak. 64: Toto 0-0 African Sports
 
Dak. 67 Kavumbagu anakosa goli la wazi kwa kupiga mpira juu huku akiwa amebaki yeye na golikipa.
 
Hawa washambuliaji wa kagera ni mbumbumbu sana sijapata kuona.
 
Hawa washambuliaji wa kagera ni mbumbumbu sana sijapata kuona.

Sure, wangekuwa makini hadi sasa Azam angekuwa amekaa si chini ya goli 3 hii ni pamoja na penati iliyopigwa na Kanoni na kuokolewa na Manula.
 
Hivi Ramadhan Singano (MESSI) Yuko Wapi!! Au Leo Amepewa Nafasi Ya Kucheza!!??? Maana Sijamsikia Kitambo!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…