Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Mchezo wa kwanza ambao ulipigwa saa 8 mchana, uliochezwa kati ya Kagera sugar dhidi ya Gwambina umemalizika kwa sare ya bao 1-1. Goli la Kagera sugar lilifungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 6, baadaye Mashack Abraham kuisawazishia timu yake dakika ya 90+1
Kwa upande mwingine Azam fc amelazimishwa kichapo cha bao 2-1 na wagosi wa kaya Coastal union mchezo uliochezwa katika Dimba la mkwakwani huko Tanga. Magoli ya Coastal union yamefungwa na Haji Ugando dakika ya 9 na Hamad Rajab dakika ya 54, huku goli pekee la Azam likifungwa na Daniel Amoah dakika ya 36.