Azam FC yamtupia vilago Mshambuliaji Yahya Mohammed raia wa Ghana

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Klabu ya Azam FC imeachana na Mshambuliaji wake Yahya Mohammed raia wa Ghana baada ya kushindwa kufanya vizuri kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.

Yahya alikuwa na mkataba wa miaka miwili na Klabu hiyo lakini kutokana na kushindwa kutimiza vizuri majukumu yake jana uongozi ulikaa na mchezaji huyo kabla ya kufikia maamuzi ya kuachana naye.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema baada ya kuondoka kwa mchezaji huyo uongozi unatafuta mbadala wake ambaye anaweza kutoka ndani au nje ya nchi.

"Ni rasmi kuanzia jana tuliachana na mchezaji wetu Yahya Mohammed baada ya makubaliano ya pande zote na leo ataondoka kuelekea kwao Ghana", alisema Jaffer.

Jaffer amesema mchezaji huyo amepewa barua yake na wamemtakia kila la heri katika maisha yake ya soka.

Mchezaji huyo alichangia kwa kasi kikubwa ubingwa wa ubingwa wa michuano ya mapinduzi iliyofanyika Zanzibar huku pia akiwa ndiye aliyefunga bao la kwanza la Azam msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…