AZAM MARINE mlete vivuko vyenu Mafia

AZAM MARINE mlete vivuko vyenu Mafia

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Kivuko MV. KILINDONI kinachotoa huduma kati ya Mafia Wilayani Mafia na Nyamisati Wilayani Kibiti Mkoani Pwani kitasimama kutoa huduma katika eneo hilo kuanzia siku ya leo Tarehe 12 Februari, 2025 ili kupisha matengenezo pamoja na kufungwa injini mpya.

Kivuko MV. KILINDONI kimewasili leo kikiwa na abiria pamoja na mizigo eneo la Nyamisati kikitokea Wilayani Mafia.

Kivuko hicho kinatarajiwa kupekekwa Mkoani Dar es Salaam ambako kitakuwa huko kwa muda wa wiki moja kikifanyiwa matengenezo hayo ili kukiongezea ufanisi kiweze kurejea kikiwa bora na salama kwa watumiaji.

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), unawaomba radhi abiria wote kutokana na usumbufu watakaoupata kutokana na kukosekana kwa huduma ya kivuko hicho.

Kwa hiyo wiki moja hakutakuwa na usafiri kwa njia ya maji, wenye uwezo wa kulipa nauli ya ndge ndio wataweza kusafiri
 

Attachments

  • 1739377205876.jpg
    1739377205876.jpg
    357.4 KB · Views: 3
Mafia usafiri ni shida sana sijajua wanapachukuliaje sjui, au ile ni kambi ya jeshi raia wameruhusiwa kuishi? ndio wilaya unayoweza ukafiwa na mazishi baada ya wiki na usiweze kwenda kuzika kama hauna nauli ya ndege
 
Mafia usafiri ni shida sana sijajua wanapachukuliaje sjui, au ile ni kambi ya jeshi raia wameruhusiwa kuishi? ndio wilaya unayoweza ukafiwa na mazishi baada ya wiki na usiweze kwenda kuzika kama hauna nauli ya ndege
tunaishi huku tunajua msoto wake. Kuishi Mafia ni zaidi ya adhabu
 
Back
Top Bottom