Nje ya mada/mada mchepuko, nimechanganya media, dishi ni la Star Times, king'amuzi ni cha Azam, chaneli za star times zinaonekana kwenye screen ya tv na zinazofunguka ni tatu TBC1, safari channel na st.guide. Je nikilipia Star times chaneli zao nitakuwa nazifungua sambamba na chaneli za azam kwenye screen moja? Nadhani hii itanipunguzia kuwa na madishi mawili/matatu na tv mbili au tatu ndani kwangu kwa kuwa media zitakuwa zinasomana kwenye tv moja bila HDM2/ HDM3
Halafu azam Media mniambie hapa vile ving'amuzi vyenu vya antenna vina shida gani? Niko Mkoani huku mbali na nyumbani, nikasema ninunue ili niangalie ligi ya Bongo!
Aisee mpaka najuta. Kila baada ya dakika chache, picha zina staki! Kwa upuuzi wenu huu ni bora nikaangalie tu mpira kwenye vibanda umiza. Siji kulipia tena.