Azam Media kuwazidi kete DStv?

Swali langu ni kuwa hata dstv huwa muda mwingine anachukua matangazo ya live from skysport....sasa kwann bakhresa asiweke ktk king'amuzi chake hizo Chanel za bein sports????

Ya hapo atakuwa amepatia sana waarabua wenzake walee
 
Swali langu ni kuwa hata dstv huwa muda mwingine anachukua matangazo ya live from skysport....sasa kwann bakhresa asiweke ktk king'amuzi chake hizo Chanel za bein sports????

Sky sports ndio anawauzia wrote hao. Anachotakiwa AZAM ni kwenda kwa Premier League(kampuni) na kununua package! Juzi juzi wameingia mkatsba mpya na sky na BT sports in pound billion! Kwahio wakitangaza kuuza tena Azam akaweke bid apewe mechi zake kadhsaa kwa msimu. Akifanya hivyo DSTV hawezi kumzuia Kama gtv
 
Sijaelewa mkuu, kwani tenda ya kuonesha EPL mpaka ipewe kampuni moja tu? DSTV si wanaweza kuendelea kuonesha na Azam na wenyewe wakapewa haki ya kuonesha:what:

Tenda huwa anapewa mmoja tu. Halafu kama Kuna mwingine inabidi aingie mkataba na aliyeshinda tenda. Kwa mfano hapa Tanzania Azam ndiye ana haki ya kuonesha Vodacom premier league ya Tanzania. Yoyote mwingine akitaka kuonesha lazima aingie mkataba na Azam tv, yaani atakuwa anamlipa Azam tv.
 

Yap tenda anapewa sky sport ko hao wengne wananunua skysport
 
Swali langu ni kuwa hata dstv huwa muda mwingine anachukua matangazo ya live from skysport....sasa kwann bakhresa asiweke ktk king'amuzi chake hizo Chanel za bein sports????
Mkuu nadhani unajua hawa wenzetu walivyogawana mkoloni na mpaka sasa kwenye biashara hali ni hiyo hiyo.

Ndio maana sehemu anazorusha bein spots dstv hamuoni.

Hapa labda Azam akubali kuwa part ya dstv yaani agawiwe mechi mfano kipindi kile tbc anarusha kurusha moja weekend tena sio kubwa ndogo.

A
 

Mkuu umesema kweli! Gharama ya haki ya kuonesha EPL live ni Kubwa mno! Na kwa sasa mwenye tenda hiyo ni Sky news ya Uingereza. Halafu yenyewe ndio huwa inaingia mkataba na makampuni mengine kama vile multi choice iliyonunua haki ya kutangaza nchi za africa chini ya sahara) sub-Saharan countries).
 
Kwa kweli umesema jambo la haki. Kila nikiangalia kwa mfano ligi ya Uholanzi (kwenye Fox Sports ya Azamtv), standard za mpira ni kubwa sana hata kuliko za huko England
Chukua team yeyote ya ligi kuu nchini uholanzi ukaichezeshe na tot ya uingereza tu mechi ya mashindano ikishinda njoo uchukue ving'amuzi vi3 vya azamtv
 
Kwa nchi za sub sahara haki ya kuonyesha epl haitolewi kwa nchi moja moja kama uko nigeria bali inatolewa kwa ukanda mzima
 
nawaza DSTV sababu nakos Champions league + epl na laliga labda,,,but star time napata BUNDESLOOGA, SERI Ana LEAGUE 1, sijajua kuhusu AZAM maana sijawahi kuwa nacho...ila AZAM NI WABUNIFU yani wakisema tu wanaonesha Champions league baasi watanikamata.....anyway si mtu wa tv sana ila sports sana hasa soccer ...hizo chanel za documentaries national geo za katuni zote au watoto etc nazipenda sana but zpataikana angalau karibia vingamuzi vyote...so good work AZAM
 
Kweli kabisa na hii ndio business strength ya company ya Azam
 
Ngumu mno.
Dstv a worldwide media ina channel rundo ambazo azam wenyewe hawazijui. Wana high capital hivyo wanaweza kuwekeza popote duniani.
Wameplant south Africa,Nigeria wanagain high profit hivyo wanainvest kwa upana na savings yao ni kubwa.
Acha kabisa dstv ni hatari.

Pia huwezi kuwaibia kiurahisi maana wana mtambo wao angani unaopitia saver zao na kingamzi vyao kila baada ya siku 7.Ina maana huwezi iba zaidi ya siku tatu kitu ambacho azam bado.
 
Sultani.
 
Hakuna kitu ambacho azam wanacho ila dstv hawana zaidi ya kurusha mpira wa bongo. Kama movie zote za dunia na bongo movie dstv ndiyo nyumbani. Tuache utani dstv ukiweza afford kile kifurushi kikubwa hutajuta katu. Acheni kufananisha mdokozi na jambazi aliyeshindikana. Dstv hata ulaya ipo halafu nyie mnatoa povuuuuu. What is azam so far.
 
Nakubali mkuu DSTV is the best
 

Dstv ipo ulaya ki vp! Inapambana kupata soko au inapatikana ukiwa na king'amuzi!? Kokote ambapo Dstv ipo basi weka king'amuzi cha Azam na yenyewe utaipata. Ata Africa Dstv haipo nchi zote (kibiashara siyo frequency kupatikana) wateja wote wa Dstv hawazidi milioni 8. Kwa maana hiyo Azam akipata wateja m5 Tz na akapata wengine m3 kutoka Ken, Rw na Ug anakua na customer base kubwa kuliko Dstv. Graph ya growth market share ya Azam ni nzuri sana. Ukiona box la azam lina enda kwa 150 na Dstv kwa 70 utaelewa zaidi. Umeme wa REA pia una mfavour sana Azm uko kijijini kila mtu akipata umeme anafunga Azam kama wana ambizana. Kumbuka umeme Tz umesambaa kwa less than 65%. Kama azam akizichanga karata vizuri ni bonge la threat kwa Dstv hasa aki anzisha movie channel ya kwake na kuonyesha ma blockbuster na akipata haki za kurusha ligi ya EPL na champions league, sababu Serie A, la liga, league 1, eredivise, standard lige (Samatta) na ligi zingine ndogo ndogo tayari zinapatikana.
*Mimi nina tumia Dstv na Azam, ila naeza ishi bila Dstv. Siwezi nika kosa kumwona mnyama kizembe.
 
Unasema akipata kibali wakati dstv anacho na East Africa yote anatamba.Unayoyasema ni probability akikosa. Vijijini kwenyewe wanajua utamu wa epl na wamefunga dstv.
Timu kama arsenal,Chelsea,man u,Liverpool man city zinajulikana vijijini kuliko maelezo.
Sema mengine siyo dstv azam ni mtoto wa nyumbani tunamheshimu lakni ktk market competition na dstv asubiri.
 
Hakunaga kama DStv, Azam TV akajifie huko!

Acha chuki mkuu, Azam ni mtanzania mwenzetu na lazima tumsifie kwa anayoyafanya ambayo hakuna mtanzania hata mmoja aliyemfikia...so tunatakiwa sisi kama watanzania tumpe support huyu ndugu yetu...kama imekuuma sana unaweza ukawapisha wengine wachangie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…