Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Azam Media Limited (AML) inasikitishwa na tangazo la kuahirishwa kwa mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kati ya Yanga SC na Simba SC ambayo ilipaswa kufanyika leo Jumamosi Machi 8, 2025 kuanzia saa 1:15 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Tukio hili limeleta athari kubwa kwa mashabiki wa soka, wateja wetu, na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla.
Hata hivyo, kama mdau mkuu wa maendeleo ya soka nchini, tumejitahidi kuhakikisha mashabiki wanapata burudani bora kupitia matangazo yetu ya moja kwa moja, lakini hali iliyojitokeza ipo nje ya uwezo wetu.
Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
Tayari timu yetu ya matangazo ikiwa na magari ya kurushia matangazo, kamera, mitambo mingine ya kurushia matangazo na timu nzima ya uzalishaji ilikuwa ipo Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mechi hiyo.