Azam media, tunaomba chonde chonde, rekebisheni kiswahili chenu cha " Baba yake na Maria!"

Azam media, tunaomba chonde chonde, rekebisheni kiswahili chenu cha " Baba yake na Maria!"

Weakman

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
995
Reaction score
1,607
Azam media imebamba hapa Tanzania!

Watanzania wanatazama na kuvutiwa na tamthilia zinazorushwa kwenye Chanel hii!

Bahati mbaya waswahili wanaonakilisha sauti kwenye tamthilia Wana shida kubwa katika tungo za kutaja undugu wa watu!

" Baba yake na Maria, badala ya Baba yake Maria!

"Shangazi yake na Kulfi, badala ya shangazi yake kulfi

Hizi tungo mbovu zinabamba mitaani, Hadi huku kwetu ambako kauli hizo hazikuwepo

Huku kwetu Mtwara watu wanaacha kauli sahihi na wanaanza kutumia kauli hizo potofu!
Hapa naamini ni mwenendo wa Tanzania kote, hivyo kufanya kuwa janga kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili

Kwakweli uongozi wa Azam uangalie hili ili kunusuru kiswahili chetu!

Pia Basata na Bakita, muliangalie hili,
Azam Ni media kubwa Sana, kiasi kwamba ina nguvu ya kukibomoa ama kukijenga kiswahili

Naomba kuwasilisha!


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom